WAPINZANI WA YANGA, MEDEAMA KUWASILI DAR ALHAMISI


Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM

WAPINZANI wengine wa Yanga SC katika mchezo wa mwisho mzunguko wa kwanza Kundi A Kombe la Shirikisho Afrika kati ya wenyeji, Medeama FC ya Ghana wanatarajiwa kuwasili Alhamisi.
Yanga watakuwa wenyeji wa Medeama FC ya Ghana Jumamosi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika mchezo wa tatu wa Kombe la Shirikisho Afrika.
Na washindi mara mbili wa Kombe la FA ya Ghana, Medeama watawasili Alhamisi Dar es Salaam kwa ndege ya Shirika la Ndege la Kenya (KQ).
Marefa wa Misri Ibrahim Nour El Din atakayepuliza filimbi akisaidiwa na Ayman Degaish na Samir Gamal Saad mdiyo watakaochezesha mchezo huo, wakati Kamisaa atakuwa Pasipononga Liwewe wa Zambia na maofisa wasimamizi ni Mfubusa Bernard ambaye atasimamia utendaji wa waamuzi wakati Mratibu Mkuu wa mchezo huo kutoka CAF atakuwa Ian Peter Keith Mc Leod.
Mchezo huo utakaoonyeshwa moja kwa moja na Azam TV, unasubiriwa kwa hamu na mashabiki wa Yanga nchini kote.
Na kurushwa moja kwa moja na Azam TV ni faraja kwa wapenzi wa timu hiyo waishio nje ya Jiji hilo ambao wataushuhudia kupitia Televisheni hiyo ya kulipia. 
Yanga inaendelea na mazoezi Uwanja wa Boko Veterani, Dar es Salaam huku ikiwa imeweka kambi hoteli Ludger Plazza, Kunduchi kujiandaa na mchezo wa tatu wa kundi lake, wakati Medeama inatarajiwa kuwasili kuanzia leo.
Yanga inahitaji ushindi dhidi ya Medeama baada ya kupoteza mechi zote mbili za mwanzo wakifungwa 1-0 mara zote – na Mo Bejaia nchini Algeria Juni 19 na TP Mazembe ya DRC Dar es Salaam Juni 28.
0

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

NAMAINGO YAZINDUA HEKA 7000 ZA MASHAMBA MJI KIJIJI CHA MSOLWA, MKURANGA

HIVI NDIVYO BIASHARA YA NGONO NAMNA INAVYOTIKISA MOROGORO: SEHEMU YA PILI.

HABARI MPASUKOOO:GARI LAGONGA WATOTO KUIKWEPA BODABODA GONGO LA MBOTO

HARAMBEE YA UJENZI HOSPITALI YA MUHEZA YAVUKA MALENGO, ZAPATIKA BIL. 1.6

WAZIRI SHONZA AMJIBU DIAMOND

HABARI MPASUKOOO!!! MCHAWI ADONDOKA AKIWA UCHI KIVULE,DAR

WAPENZI WANASANA WAKIFANYA MAPENZI GESTI

DIAMOND AITWA NA NYOTA YAJAA GOMS