WAZIRI NAPE NNAUYE AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA KARIAKOO KUFICHUA WAUZA FILAMU ZISIZO NA STIKA ZA TRA.


FI1Baadhi ya maduka yakiwa yamewekwa chini ya ulinzi kwa kuuza bidhaa za filamu na muziki zilizoingia nchini kinyume na sheria huku baadhi zikikosa stampu ya ushuru wa bidhaa ya TRA na kukosesha serikali mapato kupitia kodi na hivyo kurudisha nyuma maendeleo ya nchi.Picha na Lorietha Laurence-WHUSM.
FI2Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye(wa pili kushoto) akiwasili katika soko la kariakoo jijini Dar es Salaam ambapo alifanya zoezi la kushtukiza la  ukamataji wa  bidhaa za filamu na muziki zilizoingizwa nchini kinyume na sheria ambapo inaikosesha serikali mapato kupitia kodi na kudumaza kazi za wasanii wazawa .
FI3Mitambo ya kuzalishia bidhaa za filamu na muziki kama zilivyokutwa katika kampuni ya Aguster kariakoo jijini Dar es Salaam katika zoezi la kushtukiza la ukamataji wa bidhaa hizo zilizoingizwa sokoni kinyume na sheria na hivyo kuikosesha serikali mapato kupitia kodi.
FI4Baadhi ya bidhaa za filamu na muziki zilizokamatwa kwa  kuingizwa sokoni kinyume cha sheria kufauatia zoezi la kushtukiza la ukamataji wa bidhaa hizo ukiofanywa na Wzairi wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye kwa kushirikiana na Bodi ya Filamu Tanzania, ni Baraza la Sanaa Nchini (BASATA), Chama Cha  Hakimiliki na Hakishiriki (COSOTA) ,Taasisi ya Mapato Tanzania (TRA) pamoja na Jeshi la Polisi leo jijini Dar es Salaam.
FI5Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye( kushoto) akiangalia bidhaa za filamu na muziki zilizokamatwa katika zoezi la kushtukiza la  ukamataji wa  bidhaa hizo katika soko la Kariakoo jijini Dar es Salaam zilizoingizwa nchini kinyume na sheria, kulia ni Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bi. Joyce Fissoo.
FI6Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye(kulia)akiongea na mmoja wa wauuzaji  wa bidhaa za filamu na muziki  katika soko la Kariakoo , alipofanya zoezi la kushtukiza la ukamataji wa bidhaa hizo ambazo zilizoingia sokoni kinyume na sheria ,zoezi hilo lilifanywa kwa kushirikiana na Bodi ya Filamu Tanzania Baraza la Sanaa Nchini (BASATA), Chama Cha  Hakimiliki na Hakishiriki (COSOTA) ,Taasisi ya Mapato Tanzania (TRA) pamoja na Jeshi la Polisi
………………………………………………………………………………………………………………………………
Na Lorietha Laurence-WHUSM
Serikali imefanikwa kukamata jumla ya  bidhaa za filamu na muziki 94,000 ambapo 93,529 ni za wasanii wa nje zilizoingia nchini kinyume na sheria huku bidhaa 273 za wasanii wa ndani zikiwa hazina stampu ya ushuru wa bidhaa kutoka Taasisi ya Mapato Tanzania(TRA) zikiwa ni takwimu za awali.
Hayo yamejiri kufuatia zoezi la kushtukiza lililofanywa na Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye  leo katika soko la Kariakoo jijini Dar es Salaam na kuahidi  kwamba zoezi hilo litafanyika nchi nzima.
Aidha aliongeza kuwa mpaka sasa takribani  maduka 42 yamekaguliwa na kukamata  mitambo 19 ya kufyatua kazi za wasanii (duplicators),printer 8 za Cd/Dvd,dvd writers 31,komputa 3,ups 7 kutoka kampuni ya Aguster.
“Hatua hii ni ya mwanzo kwa kuwaonyesha Watanzania kuwa agizo la Rais wa awamu ya Tano Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli la kulipa kodi na kununua bidhaa halisi kwa kutoa risiti linasimamiwa ipasavyo”, alisema Mhe. Nnauye.
Mhe.Nnauye aliongeza kuwa wauzaji wengi wa bidhaa za filamu na muziki wamekiuka sheria  zinazosimamiwa na tasnia ya Filamu na muziki ikiwemo sheria ya Filamu na Michezo ya kuigiza na.4 ya mwka 1976 inayosimamiwa na Bodi ya Filamu Tanzania.
Waziri alizitaja sheria nyingine kuwa ni sheria ya Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) na.23 ya mwaka 1984, Sheria ya Hakimiliki na Hakishiriki  na.7 ya mwaka 1999 inayosimamiwa na Chama cha Hakimiliki na Hakishiriki ( COSOTA) pamoja na sheria ya Ushuru wa Bidhaa sura ya 147 chini ya kanuni za stampu kwa bidhaa za Filamu na Muziki ya mwaka 2013 inayosimamiwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA).
Alifafanua kuwa uchumi wa nchi na wasanii umehujumiwa sana kufuatia kuwepo kwa bidhaa za filamu zinazoingizwa nchini na kuuzwa kwa bei nafuu na kuua soko la bidhaa za ndani na kuingiza tamaduni zisizofaa katika jamii na hivyo kuchochea vitendo viovu ikiwemo ushoga.
“Bidhaa nyingi za filamu zimekuwa zikiingia nchini kwa magendo bila kulipiwa kodi na zimekuwa zikuuzwa kwa bei nafuu na hivyo kudidimiza kazi za wazawa na kuikosesha Serikali mabilioni ya fedha kupitia kodi” alisema Mhe.Nnauye.
Waziri Nnauye alitoa wito kwa Watanzania kuwa na tabia ya uzalendo kwa  kukunua bidhaa za filamu zenye stampu ya TRA  ili kusaidia katika kukusanya kodi na kuinua kipato cha wasanii.
Kwa upande wake Afisa Uhusiano wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Bw. George Haule amewaomba wananchi waunge mkono jitihada za Serikali kwa kununua bidhaa za filamu  zenye stampu ya TRA ili kusaidia kuongeza pato la kodi na kukomesha wale wote wanaokwepa kulipa kodi.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA