Waziri Ummy Mwalimu awataka Watanzania kujenga utamaduni wa kuwasaidia wazee wasiojiweza

 Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu akikagua makaziya wazee wasiojiweza ya Kilema mkoani Kagera leo
 Waziri Ummy akitoka kukagua jiko lililopo kwenye makazi hayo
 Waziri Ummy Mwalimu akisalimiana.na baadhi ya wazee waishio kwenye makazi haya
Balozi wa makazi hayo akipokea zawadi toka kwa waziri wa afya,maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto mara baada ya kuwatembelea na kujionea changamoto zinazowakabili.Waziri Ummy amewaahidi kuwachangia mfuko mmoja.wa sukari kila mwezi(picha na wizara ya afya)

Na.Catherine Sungura,Bukoba

Watanzania wametakiwa kutenga muda kwa kuwasaidia wazee waishio kwenye mazingira magumu na wale wasiojiweza

Rai hiyo  imetolewa leo  na Waziri wa afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu mara baada ya kuwatembelea wazee waishio kwenye makazi ya wazee wasiojiweza Kilima iliyopo Bukoba vijijini

Waziri Ummy amesema watanzania wengi hivi sasa hawafuati maadili ya kitanzania na utamaduni wa kusaidiana pale mtoto anapofiwa na wazazi au asiye na uwezo na kumsaidia

"Unapoona mtoto ana matatizo ni vyema kujitolea kwa kumlea kuliko kumuacha akiteseka,mzazi anajijali yeye na watoto wake tu,mtu anatupa chakula na nguo badala ya kuja kuwafariji wazee hawa, ndiyo imani na dini zetu zinavyotuambia"alisisitiza

Suala la kuwatunza wazee sio la serikali peke yake,mila za kitanzania ni kusaidiana"mtoto wa mwenzio ni wako,hivyo jamii kujenga utaratibu wa kutembelea makazi ya wazee wasiojiweza ni baraka kwa familia

Aidha,ametoa wito kwa ndugu na jamaa wenye wazee kwenye makazi yote nchini kuwachukua na kuwalea ili waepukane na adha zilizopo huko

Kwa upande wa matibabu bila malipo kwa wazee,Waziri Ummy ametoa agizo kwa Mkurugenzi wa halmashauri hiyo kuwapatia vitambulisho vya bima ya afya kwa wazee wote kumi na saba waishio kwenye makazi hayo.

Naye mzee aishiye kwenye makazi hayo John Lwiza alimuomba waziri huyo kuwasaidia chombo cha usafiri kuweza kurahisisha kuwapeleka hospitali mara wanapougua

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*