AZAM FC YATOA SARE 1-1 NA RUVU SHOOTING MABATINIIKIWA imefikisha mwezi mmoja tokea ianze maandalizi ya msimu ujao, Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, jana imetoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Ruvu Shooting katika mchezo wa kirafiki uliofanyika Uwanja wa Mabatini, Mlandizi, Pwani.
Huo ni mchezo wa saba wa kirafiki wa Azam FC, ambao ulikuwa ni mahususi kwa ajili ya benchi la ufundi chini ya Kocha Mkuu Zeben Hernandez, kukiangalia kikosi chake kitakavyokuwa kikitumia mbinu zake kwenye viwanja vibovu.
Walikuwa ni Ruvu waliotangulia kupata bao la uongozi lililofungwa kwa mkwaju wa moja kwa moja wa adhabu ndogo na Shaaban Kisiga.
Kikosi cha Azam jana Mlandizi
Azam FC inaodhaminiwa na Benki ya NMB na kinywaji cha Azam Cola, ingeweza kupata ushindi mkubwa zaidi ya huo kama si washambuliaji wake, Ibrahima Fofana, Shaaban Idd kupoteza nafasi nyingi za wazi.
Kabla mpira huo haujaenda mapumziko, katika dakika ya 44 Azam FC iliweza kusawaziha bao hilo kupitia kwa Ibrahima Fofana, aliyepiga shuti la kiufundi akiwa pembeni kidogo ndani ya eneo la 18.
Vilevile Azam FC ilianza kumfanyia majaribio mshambuliaji mpya kutoka nchini Ivory Coast, Gozano Bi Thomas, aliyetokea Africa Sports ya huko, ambaye aliingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Fofana.
Mara baada ya mchezo huo kikosi cha Azam FC kesho Jumapili kitakuwa mapumzikoni kabla ya kuendelea na mazoezi kama kawaida Jumatatu ijayo asubuhi.
0

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

HIVI NDIVYO BIASHARA YA NGONO NAMNA INAVYOTIKISA MOROGORO: SEHEMU YA PILI.

LICHA YA UZURI WAKE MWANADADA ELIZABETH MICHAEL a.k.a LULU SI MALI KITU MBELE YA RAY, AMKWEPA KUOGOPA AIBU.

IJUE HISTORIA YA UHASIMU WA KOREA KASKAZINI NA MAREKANI

WAPENZI WANASANA WAKIFANYA MAPENZI GESTI

MATOKEO YA DARASA LA SABA YATANGAZWA

PICHA:NYOKA AINA YA CHATU AUWAWA KANISANI BAADA YA KUKUTWA NYUMBANI KWA MFANYABIASHARA MAARUFU JIJINI ARUSHA AKISADIKIWA KWA IMANI ZA KISHIRIKINA

WENGI WAJITOKEZA KUMUAGA MPENDWA WAO MWANAHABARI JOYCE MMASI

KUMBE UNGA WA MUHOGO HUTENGENEZEA KIWASHIO MOTO CHA KIBIRITI