Dk. Kigwangalla afanya ziara ya kukagua vituo vya Afya Wilaya ya BundaNaibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla amefanya ziara ya kikazi katika Zahanati na vituo vya Afya katika Wilaya ya Bunda, Mkoani Mara ambapo ametoa maagizo mbalimbali yafanyiwe kazi huku suala la watumishi likibainika kuwa ni tatizo katika Wilaya hiyo.


Naibu Waziri wa Afya Dk. Kigwangalla aliweza kutembelea Zahanati ya Hunyari iliyopo Kijiji cha Hunyari, Zahanati ya Kihumbu, Maliwanda, Kituo cha Afya Mugeta, Zahanati ya Sanzate, Kituo cha Afya Ikizu.

Aidha, amewataka watendaji na Halimshahuri hiyo kuhakikisha wanakamilisha maboresho na utekelezaji mwingine ikiwemo kwa Mganga Mkuu wa Wilaya kupanga safu ya ufanyaji wa kazi kwa kuwapeleka watalaamu katika Zahanati hizo ili kuwahudumia wananchi walio pembezoni.

Kwa upande wake, Mbunge wa Jimbo la Bunda Vijijini, Mh. Boniface alipongeza ziara hiyo kwani wameweza kubaini changamoto mbalimbali zinazoikabili sehemu ya utoaji wa huduma za Afya hivyo ujio wake huo kwenye maeneo hayo ya Vijijini yamewafungua macho.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akitembelea kukagua shughuli za ufanyaji kazi wa Zahanati ya Hunyari
Jengo maalum la wodi ya Wazazi la Zahanati ya Hunyari ambalo limejengwa kwa nguvu za wananchi.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akipatiwa maelezo kutoka Mkurugenzi wa Wilaya ya Bunda namna watakavyoisaidia Zahanati hiyo
Mbunge wa jimbo la Bunda Vijijini, Mh.Boniface Mwita Getere akimtambulisha Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla pamoja na viongozi wengine akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Bunda Bi.Lydia Simeon Bupilipili.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akitoa maelezo na kupongeza wananchi wa kuweza kuchangia juhudi za ujenzi wa jengo la wodi la akinamama, Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Bunda Bi.Lydia Simeon Bupilipili.
Moja la jengo la Zahanati ya Kihumbu ambalo nalo mejengwa kwa nguvu ya wananchi kama linavyoonekana ambalo Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla aliweza kulitembelea kukagua ujenzi wake.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akitoa maagizo kwa Mganga Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Dk. Jonathan Ezekiel Budenu ( Wa tatu kulia) afanyie haraka marekebisho ya upungufu wa wafanyakazi hasa maeneo ya vijijini.
Mbunge wa jimbo la Bunda Vijijini, Mh.Boniface Mwita Getere akielezea jambo kwa wananchi wa Kijiji cha Mugeta wakati Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla alipotembelea kituo hicho cha Mugeta.
Moja ya jengo la Zahanati ya Sanzate ambalo limejengwa kwa nguvu za wananchi kama linavyoonekana pichani.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akikagua jengo hilo la Sanzate ambalo limejengwa kwa nguvu za wananchi.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akitoa maagizo kwa watendaji wa kijiji cha Sanzate.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akiwasili kijiji cha Makongoro kukagua Kituo cha Afya Ikizu.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akiwaonyesha bomba linalotakiwa kuwekwa katika chumba cha upasuaji wakati wa kuingia kwenye chumba cha upasuaji.
msafara ukiendelea.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akipatiwa maelezo namna mashine kubwa ya kisasa ya ufuaji nguo ambayo ilitolewa na Wizara ya Afya ambayo hata hivyo Kituo hicho wameshindwa kuifanyia kazi.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akionyeshwa moja ya majokofu ya kuhifadhia mahiti kwenye kituo cha Afya Ikizu.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akikabidhi Wheel chair kwa ajili ya wagonjwa wa kituo cha Afya cha Ikizu ambapo Mbunge wa jimbo hilo, Mh. Boniface Getere alizitoa kama mchango wake.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akikabidhi Wheel chair kwa ajili ya wagonjwa wa kituo cha Afya cha Ikizu ambapo Mbunge wa jimbo hilo, Mh. Boniface Getere alizitoa kama mchango wake.
ukaguzi ukiendelea
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akiaga wakati alipotembelea kwa karakana ya uchongaji ambayo ina historia ndefu.
eneo la karakana ambayo ina historia ndefu ambapo jengo hilo ndipo palipochongwa kifimb cha Hayati Mwalimu Julius Nyerere.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akiwa pamoja na viongozi wa Wilaya hiyo ya Bunda wakati wa kumaliza ziara hiyo ya kutembelea vituo vya Afya katika Wilaya ya Bunda.
0

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MATOKEO YA KIDATO CHA PILI, DARASA LA SABA YATANGAZWA ZANZIBAR

HIVI NDIVYO BIASHARA YA NGONO NAMNA INAVYOTIKISA MOROGORO: SEHEMU YA PILI.

ZAIDI YA WANANCHI 500 KUSHIRIKI MAFUNZO YA MKIKITA YA KILIMO CHA PAPAI SALAMA

MKIKITA YATOA OFA KWA KILA HEKA YA PAPAI SH. MIL. 2 KUTANDAZA MIUNDOMBINU YA UMWAGILIAJI

WATEJA WA NSSF DAR WATIMULIWA KWA MTUTU WA BUNDUKI

DIAMOND AITWA NA NYOTA YAJAA GOMS

KAMISHNA MARIJANI AZINDUA CHAMA CHA WAFUGAJI MBWA TANZANIA (TCA)

PICHA:NYOKA AINA YA CHATU AUWAWA KANISANI BAADA YA KUKUTWA NYUMBANI KWA MFANYABIASHARA MAARUFU JIJINI ARUSHA AKISADIKIWA KWA IMANI ZA KISHIRIKINA