GODFREY ZAMBI APOKEA KADI YA MFUMO WA "WOTE SCHEME" KUTOKA MFUKO WA PENSHENI WA PPF



PPF Kadi ya Wote Scheme
Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mhe. Godfrey Zambi akipokea kadi ya Mfumo wa "Wote Scheme" kupitia Mfuko wa Pensheni wa PPF kutoka kwa Meneja wa PPF kanda ya Kusini Ndg. Kwame Temu.

PPF Kadi ya Wote Scheme

Meneja wa PPF kanda ya Kusini Ndg. Kwame Temu akimueleza jambo Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Godfrey Zambi wakati wa kumkabidhi Kadi ya Mfumo wa "Wote Scheme".

PPF Kadi ya Wote Scheme
Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mhe. Godfrey Zambi akitoa neno la shukrani kwa Meneja wa PPF (Hayupo pichani) wakati wa kupokea kadi ya Mfumo wa "Wote Scheme" kupitia Mfuko wa Pensheni wa PPF.


Na. Fungwa Kilozo, Lindi
Mkuu wa mkoa wa Lindi Mhe. Godfrey Zambi ameweza kupokea Kadi ya Mfumo wa "Wote Scheme" kupitia Mfuko wa Pensheni wa PPF. 

Mhe. Zambi amepatiwa kadi hiyo ikiwa ni Siku nne tu zimepita baada ya Kujiunga na Mfumo huo katika Banda la PPF lililokuwa katika maonyesho ya Kilimo na Biashara Nane nane yaliyofanyika Kitaifa Mkoani Lindi katika Viwanja vya Ngongo.

Katika Hafla hiyo ya makabidhiano ya Kadi hiyo Mh. Zambi ameutaka Mfuko wa PPF kutanua wigo na kuwafikia wananchi wengi zaidi hasa wale wa vijijini kwani amesema kuwa mfuko huo unafaida nyingi ambazo wananchi hao ambao hawajabahatika kufika katika banda la maonyesho ya Nane nane watazikosa hasa mfumo wa "Wote Scheme" ambao hata yeye amefurahishwa nao na akaamua kujiunga.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI