HII NI KAMA FILAMU, KIMENUKA JANGWANI! WANACHAMA HAWAMTAKI MZEE AKILIMALI

Katika kile ambacho kinaonekana kama filamu sasa, sakata la mwanachama mkongwe wa Yanga, Mzee Akilimali limechukua sura mpya kwa kuwa sasa baadhi ya wanachama wenzake klabuni hapo wametaka mkongwe huyo asimamishwe uanachama.

Kauli hiyo imetolewa kwa pamoja na viongozi mbalimbali wa matawi ya Klabu ya Yanga ambao walikutana leo kwenye makao makuu ya klabu hiyo mitaa ya Jangwani ambapo wengi wao walionekana kuwa na hasira ambapo walikuwa wakizungumza kwa hisia wakidai kuwa Mzee Akilimali anawachanganya na anatakiwa kusimimishwa au kuondolewa kabisa uanachama.

Hali ilikuwa hivi Jangwani, leo asubuhi.

Mwanachama wa Yanga akifafanua jambo.
Mwanachama wa Yanga akitoa maoni yake.

Hali ipo hivi makao makuu ya Yanga.
Wakizungumza mbele ya wanaandishi wa habari na wapenzi wengine wa Yanga waliokuwa wamejaa kwenye makao makuu hayo, viongozi hao walidai kuwa kauli tata za mzee huyo zimechangia Mwenyekiti wao, Yusuf Manji kuamua kujiuzulu nafasi hiyo kamna ambavyo imekuwa ikidaiwa tangu jana.
  

Lawama nyingi zinaonekana kutupwa kwa mzee huyo ambaye mapema leo aliomba radhi kwa kauli zake tata, hata hivyo hakuwepo klabuni hapo wakati matamko hayo ya wanachama yakitolewa.

Mbali na viongozi kadhaa wa matawi, mashabiki wengi walionekana wakizunguka eneo la klabuni hapo kutaka kujua nini kinachoendelea na kama ni kweli Manji kaamua kujiuzulu au la, lakini hakukuwa na tamko la ziada tofauti na kile kilichoandikwa na mtandao huu kuwa Manji bado hajatoa tamko rasmi. 
0

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MATOKEO YA DARASA LA SABA 2013 YATOKA, YAPO HAPA ... YAONE HAPA KWA NJIA RAHISI KABISA

MATOKEO YA DARASA LA SABA YATANGAZWA

HIVI NDIVYO BIASHARA YA NGONO NAMNA INAVYOTIKISA MOROGORO: SEHEMU YA PILI.

MBUNGE MOLLEL AITAKIA NAMAINGO MAFANIKIO MEMA 2019

JIONEE WAREMBO KUMI WA NGUVU AFRIKA MASHARIKI

HIZI NDIO DALILI ZA VVU KWA WATOTO WADOGO

ANGALIA PICHA WADADA HAWA WALIVYOPIGWA