KATIBU MKUU WA CHADEMA MKOANI MWANZA , JOHN NWALILE AITOSA CHADEMA AJIUNGA NA CCM ,APINGA OPERESHENI UKUTA



KATIBU Mkuu wa CHADEMA mkoani Mwanza, John Nwalile (pichani kati), ametangaza kukihama chama hicho na kujiunga na CCM mapema leo Agosti 30, 2016. 
Akitangaza uamuzi huo mbele ya waandishi wa habari, alisema sababu kubwa aliyoitaja iliyomsukuma kukihama CHADEMA, ni pamoja na kutokuwa na sababu ya msingi ya kutomuunga mkono Rais John Pombe Magufuli katika jitihada zake za kujenga misingi mipya ya nchi ikiwa ni pamoja na kupambana na wala rushwa na kuimarisha uwajibikaji miongoni mwa watumishi wa umma. Pia Nwalile amesema, sababu nyingine ni kupinga mpango wa Operesheni UKUTA iliyotangazwa nchinzima na Kamati Kuu ya CHADEMA ambayo imepangwa kuanza Septemba Mosi mwaka huu 2016. 
Ikiwa imebaki siku moja tu kuanza kwa operesheni hiyo, kujitoa kwa kiongozi huyu wa juu kabisa wa CHADEMA kwenye mkoa wenye ushawishi mkubwa kisiasa hapa nchini ni pigo kubwa kwa chama hicho katika mkakati wake mpya wa UKUTA. 


Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI