LOWASSA APIGWA STOP KUENDELEA NA ZIARA MBEYA


 Edward Lowassa akipata maelezo mbalimbali kutoka viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama kutoka napolisi kuuzuia kikao cha ndani cha Mh.Edward Lowassa na wanachama wa Chadema wa wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya ambacho kilizuiwa kufanyika na Jeshi la Polisi asubuhi ya leo.
   Sehemu ya askari polisi wakiwa kwenye eneo ambalo lilitegemewa kufanyika kikao cha ndani cha Mh.Edward Lowassa na wanachama wa Chadema wa wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya ambacho kilizuiwa kufanyika na Jeshi la Polisi asubuhi ya leo.
  Edward Lowassa akiondoka na msafara wake baada ya kupata maelezo mbalimbali kutoka viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama kuzuiwa kufanyika kwa kikao cha ndani cha Mh.Edward Lowassa na wanachama wa Chadema wa wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya ambacho kilizuiwa kufanyika na Jeshi la Polisi asubuhi ya leo.

  Baadhi ya Wananchi wakitazama tukio hilo
 --
By Lauden Mwambona, Mwananchi
Mbeya. Msafara wa aliyekuwa mgombea wa Urais kupitia Chadema, Edward Lowassa umekwama kwenda Mikoa ya Rukwa na Katavi  baada ya polisi kuuzuia kwa hofu kwamba unaweza kuingilia ziara ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa anayetembelea mikoa hiyo.

Lowassa ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema alianzia ziara yake  mkoani hapa tangu Agosti 21 na juzi alifanya vikao vya ndani katika majimbo yanayoshikiliwa na wabunge wa chama chake  mkoani  Songwe wakati leo asubuhi alitarajiwa kwenda Katavi na Rukwa.

Katika Mikoa ya Rukwa na Katavi alitarajiwa kufanya mikutano ya ndani Majimbo ya  Nkasi Kaskazini na Kusini na Sumbawanga.

Katibu wa Chadema Kanda ya Nyanda za Juu Kusini wanayoiita ‘Kanda ya Nyasa’, Frank Mwaisumbe  alisema  kwamba polisi walimpigia simu Lowassa juzi saa 1.00 jioni akiwa Tunduma  wakimtaka aahirishe ziara yake Mkoa wa Rukwa.

Kamanda wa polisi Mkoa wa Rukwa, Gorge Kyando alipoulizwa  kwa njia ya simu alisema waliwashauri viongozi wa Chadema wapange siku nyingine ya ziara kwa sababu  mkoa ulikuwa na ugeni mkubwa.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

ALLY KAMWE AZIMIA KWA MKAPA.

RAIS SAMIA KUZINDUA MKUTANO MKUU WA 79 WA BARAZA LA MICHEZO YA MAJESHI DUNIANI

MIGINGO KISIWA KIDOGO ZAIDI AFRIKA KILICHOGOMBEWA NA UGANDA, KENYA