MAJALIWA ATOA ZAWADI KWA WASHINDI WA NANE NANE KANDA YA NYANDA ZA JUU KUSINI


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi ngao ya  Ushindi wa pili katika kundi la Tasisi na Mashirika ya serikali na yasiyo ya serikali, Mkuu wa Magereza wa Mkoa wa Mbeya, Julius Sang'unda  wakati alipofunga Maonyesho ya Wakulima Nanenane kwenye uwanja wa John Mwakangale jijini Mbeya Agosti 8, 2016.  Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos makalla na wapili kulia kwake ni Naibu  Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson. Kulia ni Mwenyekiti wa TASO wa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Crispin  Mtono .  (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi ngao ya ushindi wa tatu katika kundi la Tasisi na Mashirika ya serikali na yasiyo ya serikali, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mpango wa Uendelezaji Kilimo katika Eneo la Ukanda wa kusini mwa Tanzania  (SAGCOT), Geofrey Kirenga  wakati alipofunga Maonyesho ya Wakulima Nanenane kwenye uwanja wa John Mwakangale jijini Mbeya Agosti 8, 2016. Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos makalla na wapili kulia kwake ni Naibu  Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson. Kulia ni Mwenyekiti wa TASO wa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Crispin  Mtono.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifurahia picha yake iliyochorwa na kutolewa kwake na Chama cha Wandishi wa Habari za Utalii na Uwekezaji Tanzania mkoani Mbeya (TAJATI) katika kilele cha sherehe za Maonyesho ya wakulima Nanenane   kwenye uwaja wa wa John Mwakangale jijini Mbeya Agost 8, 2016. Watatu kulia kwake ni mkewe Mary na wapili kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akionyesha karoti zilizostawi vizuri wkati alipotembelea banda  la Mapanda Mkoani Katavi katika maonyesho ya wakulima Nanenane  kwenye uwanja wa John Mwakangale jijini Mbeya Agosti 8, 2016.   Kulia kwake ni mkewe Mary
 Waziri Mkuu,  Kassim Majaliwa akitazama vitunguu vilivyopandwa kwenye gunia namna ya kilimo  ambacho ni muafaka  kwa watu waishio mijini hasa magorofani. Alikuwa akitembela maonyesho ya wakulima Nanenane kwenye uwanja wa Maonyesho wa John Mwakangale wa jijini Mbeya
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakitazama  jiko banifu linalotumia gesi ya pumba  wakati alipotembelea  banda la Magereza kwenye maonyesho ya Wakulima Nanenane  katika uwanja wa  John Mwakakangale  jijini Mbeya  Agosti 8, 2016. 
 
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na askari magereza wa mkoa wa Mbeya baada ya kutembelea  banda lao kwenye maonyesho ya wakulima Nanenane kwenye  uwanja wa  John Mwakangale jijini Mbeya Agosti 8, 2016.  Kulia ni Mkuu wa Magereza mkoa  wa Mbeya Julius Sang’unda
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa   na mkewe Mary wakiwa katika picha ya pamoja na vijana wa kujitolea kutoka Uingereza ambao Agosti 8, 2016 walitembelea maonyesho  ya wakulima Nannane kwenye uwanja wa John Mwakangale  jijini Mbeya
  Baadhi ya viongozi  waliohudhuria kwenye kilele cha Maonyesho ya Wakulima Nanenane katika uwanja wa John Mwakangale  jijini Mbeya wakimsikiliza  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipohutubia Agosti 8, 2016
 Baadhi ya viongozi  waliohudhuria kwenye kilele cha Maonyesho ya Wakulima Nanenane katika uwanja wa John Mwakangale  jijini Mbeya wakimsikiliza  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipohutubia Agosti 8, 2016
0

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

NAMAINGO YAZINDUA HEKA 7000 ZA MASHAMBA MJI KIJIJI CHA MSOLWA, MKURANGA

HIVI NDIVYO BIASHARA YA NGONO NAMNA INAVYOTIKISA MOROGORO: SEHEMU YA PILI.

HABARI MPASUKOOO:GARI LAGONGA WATOTO KUIKWEPA BODABODA GONGO LA MBOTO

HARAMBEE YA UJENZI HOSPITALI YA MUHEZA YAVUKA MALENGO, ZAPATIKA BIL. 1.6

WAZIRI SHONZA AMJIBU DIAMOND

HABARI MPASUKOOO!!! MCHAWI ADONDOKA AKIWA UCHI KIVULE,DAR

WAPENZI WANASANA WAKIFANYA MAPENZI GESTI

DIAMOND AITWA NA NYOTA YAJAA GOMS