MAKAMU WA RAIS MAMA SAMIA SULUHU HASSAN AITAKA TAASISI YA HANS SEIDEL FOUNDATION ISADIE KUPELEKA ELIMU YA URAIA BUNGENI


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania SAMIA SULUHU HASSAN ameitaka Taasisi ya Hans Seidel Foundation isaidie kupeleka elimu ya uraia bungeni ili wabunge wajue wajibu wao ndani na nje ya Bunge. 
Mheshimiwa SAMIA ametoa kauli hiyo leo baada ya kukutana na ujumbe wa Taasisi ya Hans Seidel Foundation uliomtembelea ofisi kwake Ikulu, Jijini Dar es salaam kutaka kujua kama ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuna sheria na kanuni za kuendesha vikao vya Bunge. Makamu wa Rais aliueleza ujumbe huo ulioongozwa na Mwenyekiti wa Hans Seidel Foundation Prof. URSULA MANNK kuwa sheria na kanuni zipo za kuendesha vikao vya Bunge lakini baadhi ya wabunge hawazifuati kama inavyotakiwa. Alisema kwa mtazamo wake elimu ya uraia itasaidia katika kuwafanya wabunge hao wajenge nidhamu katika michango na ushiriki wao kwa ujumla ndani na nje ya Bunge. 
Akizungumzia kuhusu kuanzishwa kwa dawati la jinsia katika vituo vya polisi Mheshimiwa Samia alisema ni hatua nzuri kwani wanawake kwa sasa wako huru kueleza wanapofanyiwa ukatili wa kijinsia tofauti na ilivyokuwa hapo awali. 

"Kwa sasa wanawake wanakutana na wanawake wenzao wako huru kuzungumza wanaporipoti matukio ya kupigwa na haki inatendeka bila ya hata kutoa rushwa. Kuna mabadiliko ndani ya Jeshi la Polisi kwa upande huo," alisema SAMIA 

Alisema kazi kubwa inayofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano ni kuhakikisha watu wote wanaoenda kinyume na taratibu wanachukuliwa hatua za kisheria na kusema kwenye utumishi wa umma mambo yamebadilika kiasi kwamba makusanyo ya kodi yameongezeka serikalini. 

Taasisi ya Hans Seidel Foundation yenye makao yake makuu Munich, nchini Ujerumani ambayo inajishughulisha na masuala ya demokrasia, amani na maendeleo huku ikitoa kipaumbele kwenye elimu ya uraia inaendesha shughuli zake katika nchi zaidi ya 60 duniani. 

Imetolewa na Ofisi ya Makamu wa Rais 
Dar es salaam11/08/2016

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.