4x4

MAMIA YA WAKAZI MJI WA MBALIZI WAJITOKEZA KUELEZA KERO KWA MKUU WA MKOA WA MBEYA


Awaonya na kuwataka kuacha mara moja wanaochochea Mgogoro wa kisiasa Mbalizi Alipatia ufumbuzi tatizo la Maji mbaliziAwapa wiki mbili halmashauri kumaliza sitonfaumu kati yao na bodaboda na wafanyabiashara wa masoko
- Serikali inakusudia kufufua viwanda vya Tanganyika Packers na Mbeya textile
MAMIA YA wakazi wa mji wa Mbalizi wamejitokeza kueleza Kero mbalimbali kwa Mkuu wa mkoa wao huku Kero Nyingi zikihusisha tatizo la Maji, Mgogoro wa kisiasa ndani ya Mamlaka YA mji Mdogo, mvutano wa halmashauri na wafanyabiashara wa masoko A&B , ufufuaji viwanda na ujenzi wa ofisi ya halmashauri
Akijibu Kero za wananchi Mkuu wa Mkoa amekwenda na kuwaonya wote wanaochochea Mgogoro wa kisiasa ndani ya mamlaka vya mji Mdogo na amemwagiza Mkuu wa wilaya, mkurugenzi na viongozi wa Mamlaka kukaa pamoja na kuelekezana majukumu yao , kuelewa sheria na kutekekeza majukumu yao kwa mujibu wa sheria na si kwa mihemuko YA kiitikadi
Amehaidi kumchukulia hatua yeyote Yule atakayekiuka miongozo itakayotolewa na amewataka wanasiasa kutokuendekeza Siasa kwani kufanya hivyo ni kuwagawa wananchi na kuwacheleweshea maendeleo
Kuhusu tatizo la Maji mji wa Mbakizi amewaagiza Mamlaka YA Maji Mbeya kukaa na Mamlaka ya mji Mdogo mbalizi kuingia makubaliano ili Mamlaka ya Maji Mbeya wahudumiwe eneo la jiji na Mamlaka ya Mbalizi na kwa kufanya hivyo tatizo la Maji litakuwa limekwisha kwani Mamlaka ya Maji Mbeya wana Maji YA kutosha, watalaam, vitendea kazi YA kuboresha huduma YA Maji 
Kuhusu viwanda vya Tanganyika Packers na Mbeya Textile amesema nia YA serikali ni kuvifufua na kazi iliyopo ni kutafuta wawekezaji . Kufunguliwa kwa viwanda hivyo kutaongeza ajira na masoko kwa Pamba na mifugo
Kuhusiana na Azma YA halmashauri kuwachukulia hatua bodaboda na wafanyabiashara kutakiwa kuachia vyumba sokoni amewagiza kukaa na kufikia muafaka ikiwemo kutoa Elimu kwanzana kabla
Post a Comment