4x4

MBUNGE WA MBINGA MJINI MAPUNDA AAHIDI KUKARABATI NYUMBA YA KUISHI ASKARI WAGENI

 Mbunge wa Jimbo la Mbinga Mjini, Sixtus Mapunda (katikati) akiwa na maofisa wa Polisi wilaya ya Mbinga alipotembelea leo makao makuu ya Polisi Wilaya Mbinga na kupokelewa na OCD, SSP Ramia Mganga. Amezisikiliza kero zao na kuahidi kushirikiana na wenzake kuezeka nyumba ya Polisi wageni na kuanza mchakato wa kujenga bwalo la Polisi Mbinga.

 Askari wakiimba wimbo wa utii na uaminifu Kwa nchi
 OCD, SSP Ramia Mganga akiniongoza kwenda kuiangalia nyumba ya askari wageni wanapoishi kabla ya kupata makazi ya kudumu.
Mbunge wa Jimbo la Mbinga Mjini, Sixtus Mapunda (kulia) akiangalia nyumba ya askari wageni ambayo ambayo ameahidi  tutashirikiana nao kuikarabati.
Post a Comment