NDEGE YA URUSI YATUNGULIWA NA KUUA 5 SYRIA





Ndege ya kijeshi ya Urusi aina ya Mi-8 ikiteketea baada ya kutunguliwa.



Wananchi wakishuhudia mabaki ya ndege hiyo ya kijeshi.
Ndege ilitungulia ni sawa na hii hapo juu.
WATU watano wamepoteza maisha baada ya ndege ya kijeshi ya Urusi aina ya Mi-8 kutunguliwa na waasi kaskazini mwa Syria, maofisa wa Urusi wameeleza.
Kwa mjibu wa Wizara ya Ulinzi, ndege hiyo aina ya Mi-8, ilikuwa na watu watano; wafanyakazi watatu wa ndege hiyo na maofisa wawili wa kijeshi wakati ilipoangushwa katika Jimbo la Idlib.
Msemaji wa Ikulu ya Rais wa Urusi, Kremlin, amesema kuwa watu hao wote watano wamefariki dunia.Ndege hiyo ilikuwa ikirudi baada ya kupeleka msaada wa kibinaadamu huko Aleppo.
Kwa mujibu wa kitengo cha habari cha Interfax cha Urusi, kimemnukuu ofisa mmoja akisema haijulikani ni kundi gani lililoiangusha ndege hiyo.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI

KOCHA WA AL.AHLY ASEMA YANGA NI TIMU BORA NA NGUMU