RAIS DKT. MAGUFULI AWEKA JIWE LA MSINGI DARAJA WA WAENDA KWA MIGUU LA FURAHISHA PAMOJA NA UPANUZI WA BARABARA YA MWANZA AIRPORT


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mkewe Mama Janeth Magufuli pamoja na Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Edwin Ngonyani, Mbunge wa Sumve Richard Ndassa wakipiga makofi mara baada ya tukio la uwekaji wa Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Daraja la waenda kwa miguu la Furahisha pamoja na Upanuzi wa barabara ya Mwanza-airport.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katikati akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Mitambo itakayotumika katika ujenzi wa Daraja la waenda kwa miguu la Furahisha pamoja na upanuzi wa barabara ya Mwanza-airport.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini TANROADS, Mhandisi Patrick Mfugale akitoa maelezo ya namna daraja la Furahisha litakavyokuwa mara baada ya kukamilika.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia maelfu wa Wakazi wa Mwanza na vitongoji vyake mara baada ya kuzindua ujenzi wa Daraja la Furahisha jijini Mwanza
Wanachi wakishangilia wakati Rais Dkt. Magufuli alipokuwa akihutubia.
Mwanamuziki Christian Bella akisalimiana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya kutumbuiza katika uwanja wa Furahisha jijini Mwanza.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Edwin Ngonyani ,Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella, Mke wa Rais, Mama Janeth Magufuli pamoja na Mbunge wa Ilemela Angelina Mabula wakiomba dua kabla ya kuhutubia maelfu wa wakazi wa jiji la Mwanza.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Edwin Ngonyani, Waziri wa Kilimo Mhandisi Charles Tizeba na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongela wakiimba Wimbo wa Taifa kabla ya kuhutubia maelfu ya wakazi wa jiji la Mwanza. PICHA NA IKULU.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA