SAMATTA KAZINI TENA LEO EUROPA LEAGUE


Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta leo anatarajiwa kuiongoza timu yake, KRC Genk ya Ubelgiji katika mchezo wa kwanza hatua ya mwisho ya mchujo wa kuwania tiketi ya kuingia kwenye makundi ya Europa League dhidi ya Lokomotiva Zagreb ya Croatia.
Genk wamesafiri hadi Zagreb kwa mchezo wa kwanza leo, wakati marudiano yatakuwa Alhamisi ya Agosti 25 Uwanja wa Luminus Arena, Genk na mshindi wa jumla atafuzu hatua ya makundi moja kwa moja, ambako atapangwa na vigogo wa Ulaya.
Genk imefika hatua hii baada ya kuitoa Cork City FC ya Ireland kwa ushindi wa jumla wa 3-1, baada ya kushinda 1-0 nyumbani na 2-1 ugenini.
Mbwana Ally Samatta leo anatarajiwa kuiongoza timu yake, KRC Genk ya Ubelgiji katika mchezo wa kwanza hatua ya mwisho ya mchujo wa kuwania tiketi ya kuingia kwenye makundi ya Europa League dhidi ya Lokomotiva Zagreb ya Croatia.

Na Genk wataingia kwenye mchezo huo wakitoka kulazimishwa sare ya 2-2 nyumbani na Waasland-Beveren Jumamosi na kufungwa 1-0 ugenini na Gent Uwanja wa Ghelamco-Arena mjini Gent katika mfululizo wa Ligi Daraja la Kwanza A Ubelgiji.
Samatta ambaye Desemba 13 mwaka huu atafikisha miaka 24, alijiunga na Genk Januari mwaka huu kutoka TP Mazembe ya DRC, iliyomtoa Simba SC ya Tanzania mwaka 2011.
Na baada ya mafanikio makubwa akiwa na klabu ya Lubumbashi ikiwemo kushinda taji la Ligi ya Mabingwa Afrika na kuwa mfungaji bora wa michuano hiyo sambamba na kushinda tuzo ya Mwanasoka Bora Anayecheza Afrika, Samatta akahamia Ulaya Januari mwaka huu.
Na tangu atue Genk, Samatta amecheza jumla ya mechi 25 za mashindano yote, zikiwemo 18 za msimu uliopita na tatu za msimu huu hadi sasa, kati ya hizo nne ni za Europa League msimu huu.
Katika mechi hizo ni 10 tu ndiyo alianza, nyingine zote akitokea benchi na ameweza kufunga mabao saba, moja tu katika Europa League.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*