SERIKALI YALIFUNGIA GAZETI LA MSETO KWA MIEZI 6
NA SHAMIMU NYAKI WHUSM
WAZIRI wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye, (pichani), amelifungia gazeti la Mseto   kwa miezi 36 kutokana na kuchapisha habari za uongo na kugushi kwa kutumia nyaraka mbalimbali za Serikali.
Uamuzi huo wa kulifungia gazeti la Mseto  umetolewa kwa Tangazo la Serikali Na. 242 lilitolewa tarehe 10Agosti 2016 kwa mujibu wa Sheria ya Magazeti ya mwaka 1976 Sura ya 229,Kifungu 25(1).
Mhe. Nape Moses Nnauye ameeleza kuwa Kifungu hicho kinampa mamlaka yeye kama Waziri kuchukua uamuzi wa kufungia Gazeti kutokana na mwenendo wa uandishi wa gazeti hilo wa kuandika na kuchapisha habari za uongo na kugushi kwa kutumia nyaraka mbalimbali za Serikali.
“Serikali kwa masikitiko makubwa imelazimika kilifungia gazeti la Mseto  kutokana na mwenendo wa uandishi wa kuandika na kuchapisha habari za uongo na kugushi kwa kutumia nyaraka mbalimbali za Serikali kwa nia ya kumchafua Rais  wetu wa Awamu ya Tano Mhe.Dkt.John Pombe Mgufuli na viongozi wa Serikali” Alisema Mhe Waziri Nape.
Aidha Mhe. Nape amesema kuwa hatua ya kulifungia gazeti la Mseto imechukuliwa baada ya Msajili wa Magazeti kufanya juhudi kubwa za muda  mrefu kuanzia Septemba,2012 hadi Agosti,2016 kumtaka Mhariri wa gazeti hilo kuacha kuandika  habari za upotoshaji,uchochezi na za uongo na zisizo zingatia maadili ya taaluma ya uandishi wa Habari bila mafanikio.
Ameongeza kuwa Serikali ya Tanzania imeridhia mikataba mbalimbali ya Kimataifa inayoanisha Uhuru wa Habari na mipaka ya habari kama vile tamko la Haki za Binaadamu la mwaka 1948 ambapo nchi yetu imeruhusu kwa kiwango kikubwa  kwa kuweka ukomo wa uhuru huo kwa kukataza habari za uzushi uongo na uchochezi.
Gazeti la Mseto limezuiwa kuchapishwa katika njia nyingine yeyote ikiwemo mitandao (Online publication) kwa mujibu wa Sheria ya Mawasiliano ya  Kieletroniki na Posta Sura ya 306.


Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Moses Nnauye akizungumza na waandishi wa Habari kuhusu kulifungia gazeti la Mseto kwa miezi 36 leo Agosti 11,2016 katika ukumbi wa Wizara hiyo Jijini Dar es Salaam kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari MAELEZO  Bw.Vicent Tiganya
Mkutano ukiendelea
0

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MATOKEO YA KIDATO CHA PILI, DARASA LA SABA YATANGAZWA ZANZIBAR

HIVI NDIVYO BIASHARA YA NGONO NAMNA INAVYOTIKISA MOROGORO: SEHEMU YA PILI.

ZAIDI YA WANANCHI 500 KUSHIRIKI MAFUNZO YA MKIKITA YA KILIMO CHA PAPAI SALAMA

MKIKITA YATOA OFA KWA KILA HEKA YA PAPAI SH. MIL. 2 KUTANDAZA MIUNDOMBINU YA UMWAGILIAJI

WATEJA WA NSSF DAR WATIMULIWA KWA MTUTU WA BUNDUKI

PICHA:NYOKA AINA YA CHATU AUWAWA KANISANI BAADA YA KUKUTWA NYUMBANI KWA MFANYABIASHARA MAARUFU JIJINI ARUSHA AKISADIKIWA KWA IMANI ZA KISHIRIKINA

KAMISHNA MARIJANI AZINDUA CHAMA CHA WAFUGAJI MBWA TANZANIA (TCA)

MATOKEO YA DARASA LA SABA YATANGAZWA