SONG AENDA KUMALIZIA SOKA YAKE RUBIN KAZAN


KLABU ya Rubin Kazan ya Urusi imemsajili kiungo wa kimataifa wa Cameroon, Alex Song ambaye alikuwa huru.
Hata hivyo, tangazo la usajili wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 katika tovuti ya klabu hiyo halijazama kwa undani juu ya mkataba.
Song ameichezea mechi 49 timu ya taifa ya Cameroon na amechezea klabu zote Arsenal, alikodumu kwa miaka sita na Barcelona.
Kiungo huyo aliibukia kwenye kikono ya kocha Mfaransa, Arsene Wenger baada ya kujiunga na The Gunners kwa mkopo kwanza mwaka 2005, na akacheza mechi zaidi ya 150 katika klabu hiyo kabla ya kwenda hispania mwaka 2012. 

Rubin Kazan ya Urusi imemsajili kiungo wa kimataifa wa Cameroon, Alex Song aliyewahi kucheza Arsenal na Barcelona

Hata hivyo, akashindwa kupata namba ya kudumu kwenye kikosi cha kwanza cha Wakatalunya, hatimaye akatemwa baada ya kucheza mechi 65 tu za mashindano zote ndani ya miaka minne.
Kiungo huyo mkabaji pia alicheza kwa misimu miwili kwa mkopo West Ham baada ya kushindwa Barcelona.
Mwishoni mwa Mei, kocha wa zamani wa Malaga, Javi Gracia akaajiriwa na klabu hiyo kama kocha Mkuu, kufuatia kumaliza nafasi ya 10 kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Urusi na ndiye anayemsajili Song.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI