USHINDI WA MEDEAMA DHIDI YA MAZEMBE WAITUPA NJE YANGA KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA





Wawakilishi pekee wa Tanzania kwenye michuano ya kimataifa Yanga SC, wametupwa nje kwenye Michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika, baada ya TP Mazembe kuchapwa mabao 3-2 na Medeama ya Ghana katika mchezo wa kundi A uliofanyika kunako dimba la Essipong huko Sports Takoradi, Ghana.Medeama walipata mabao yao kupitia kwa Enock Atta Agyei, Moses Amponsah Sarpong na Kwesi Donsu huku Mazembe wakipata mabao yao yote mawili kupitia kwa Jonathan BolingiKufuatia matokeo hayo, Medeama ambao mchezo wa mwisho watacheza na MO Bejaia ya watahitaji sare ya aina yoyote ili kufuzu hatua ya nusu fainali, wakati huo Yanga watakuwa ugenini wakikipa na TP Mazembe mjini Lubumbashi, mchezo ambao utakuwa ni wa kukamilisha ratiba tu kwa upande wa Yanga.
Mpaka sasa, TP Mazembe bado wako kileleni na pointi zao 10 baada ya michezo mitano, wakishinda mara tatu, sare mara moja na kufungwa mara moja, wakifuatiwa kwa karibu na Medeama wenye alama nane, Bejaia wakishika nafasi ya tatu na pointi zao tano na Yanga wakiburuza mkia na pointi zao nne.- 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*