Waziri Mahiga atembelewa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa.


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Augustine Mahiga (Mb.), akimpokea rasmi Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa Mhe. Jean-Marc Ayrault (kushoto) alipotembelea Wizarani katika ziara yake ya kikazi nchini. Mazungumzo kati yao yalijikita katika kuimarisha ushirikiano baina ya Tanzania na Ufaransa ili kuchangia  maendeleo ya nchi hizi mbili. Pia Waziri Mahiga alitumia fursa  hiyo kumpa salamu za pole kutokana na mashambulio ya kigaidi yaliyotokea nchini Ufaransa hivi karibuni. Mazungumzo hayo yalifanyika  katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Jijini Dar es Salaam tarehe 02 Agosti, 2016.
Waziri Mahiga akizungumza huku Mhe. Waziri Ayrault akimsikiliza.
Wajumbe waliofuatana na Mhe. Waziri Aryault nao wakifuatilia mazungumzo. Kulia ni Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Mhe. Malika Berak
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa, Mhe. Jean-Marc Ayrault akifafanua jambo wakati wa mazungumzo yake na Mhe. Mahiga alipotembelea Wizarani leo.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Mindi Kasiga (kulia) na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika, Bi. Mona Mahecha nawakifuatilia mazungumzo hayo kwa makini. 
Mazungumzo yakiendelea
Waziri Mahiga na mgeni wake Waziri Ayrault wakiwa katika picha ya pamoja.
Waziri Mahiga akiagana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa Mhe. Ayrault mara baada ya kumaliza mazungumzo yao. 
0

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

HIVI NDIVYO BIASHARA YA NGONO NAMNA INAVYOTIKISA MOROGORO: SEHEMU YA PILI.

DC MJEMA AONJA ADHA YA MAFURIKO AKIKAGUA ATHARI ZA MAFURIKO ILALA

ZAKIA MEGHJI AWATIA HAMASA GIRL GUIDES, ATAKA WAWE JASIRI

DC MKURANGA AZINDUA MRADI WA MASHAMBA MJI YA NAMAINGO MSOLWA

WAPENZI WANASANA WAKIFANYA MAPENZI GESTI

TGGA WAMUAGA BOSS WA GIRL GUIDES AFRIKA KWA HAFLA KABAMBE

IJUE HISTORIA YA UHASIMU WA KOREA KASKAZINI NA MAREKANI

ANGALIA PICHA NDEGE KUBWA YA ABIRIA DUNIANI ILIYOANZA SAFARI NDEFU ZAIDI!

Wasafi TV kuanza kurusha matangazo yake leo (+video)