WAZIRI MKUU AWATAKA WAFUGAJI WAKUBWA KUJIANDAA KUFUGA KISASA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkewe  Mary wakiteremka kuelekea eneo la kuchinjia ng’ombe katika kiwanda cha nyama Ngulu Hills Ranch kilichopo Morogoro wakati walipokitembelea kiwanda hicho Agosti 3, 2016. (Picha na  Ofisi ya Waziri Mkuu)
war2Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary (kulia) wakikagua eneo la kuchinjia ng’ombe katika kiwanda cha nyama cha Nguru Hills Ranch cha Morogoro  Agosti 3, 2016.  Kushoto ni Mkurugenzi na Mshauri wa Kiwanda hicho, Danstan Mrutu. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
war3Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkewe Mary wakizingumza na Mkurugenzi na mshauri wa kiwanda cha nyama cha Ngulu Hills Ranch cha Morogoro , Dunstan Mrutu (kulia kwa Waziri mkuu) )  wakati walipokitembelea kiwanda hicho Agosti 3, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
war4Watoto na wananchi wa kijiji cha Majichumvi  wilayani Mvomero wakionyesha mabango wakati WaziriMkuu,Kassim Majaliwa aliposimama kijijini kwao kuwasikiliza Agosti 3, 2016.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
war5Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary  (kulia) wakipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pesheni wa LAPF, Eliud Sanga wakati alipokagua ujenzi wa stendi  mpya ya Msamvu Morogoro Agosti 3, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
war6Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua jengo la Stendi mpya ya mabasi la Msamvu mjini Morogoro Agosti 3, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
war7Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi wa Mjini  Morogoro baada ya kukagua ujenzi wa stendi mpya ya Msamvu Agosti 3, 2016. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt.Stephene Kebwe na kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF,Eliud Sanga. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
war8Awamu ya kwanza ya jengo la stendi mpya ya mabasi ya Msamvu mjini Morogoro iliyokamilika kwa asilimia 90. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aliitembelea stendi hiyo na kuzungumza na wadau Agosti 3, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
war9Waziri mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza Bibi Halima Mwishehe alipouliza swali wakati Waziri Mkuu alipozungumza na Wananchi kwenye stendi mpya ya Msamvu Morogoro baada ya kukagua ujenzi wake Agosti 3, 2016.  Kulia ni Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Dkt. Stephene Kebwe. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
war10WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka wafugaji wenye mifugo mingi nchini kujiweka tayari kwa ajili ya kuhamia kwenye maeneo yatakayotengwa na Serikali katika ranchi mbalimbali nchini ili waweze kufuga kisasa.
Pia aliwataka wafugaji hao kushirikiana na Serikali katika kuboresha miundombinu ya maeneo hayo ikiwemo ujenzi wa visima vya maji na majosho ili ufugaji wao uwe na tija.
Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Jumatano, Agosti 03, 2016) wakati alipotembelea kiwanda cha kusindika nyama cha Nguru Hills Ranch kilichoko wilayani Movomero.
Hata hivyo Waziri Mkuu alisema kitendo cha wafugaji hao kuhamia katika ranchi kitawezesha mifugo yao kuwa na ubora kwa sababu aina ya ufugaji wa sasa ya kutembeza mifugo umbali mrefu inasababisha ufugaji wao kuwa na tija ndogo.
Akizungumzia kuhusu uwepo wa kiwanda cha kuchakata nyama wilayani Mvomero Waziri Mkuu alisema kitamaliza mgogoro wa muda mrefu kati ya wakulima na wafugaji kwa kuwa wafugaji watapata fursa ya kuuza mifugo yao kiwandani hapo.
“Uwepo wa viwanda katika maeneo yetu utatuwezesha kupunguza matatizo tuliyonayo katika maeneo yetu ikiwemo suala la migogoro kati ya wafugaji na wakulima. Viwanda ndiyo vitakavyotuondoa kutoka katika uchumi wa chini hadi wa kati,” alisema.
Kwa upande wake Mkurugenzi na Mshauri wa kiwanda cha Nguru Hills Ranch, Dunstan Mrutu alisema kiwanda hicho chenye uwezo wa kuchinja ng’ombe 300, mbuzi na kondoo 1,500 kwa siku kinatarajiwa kufunguliwa mwezi Desemba mwaka huu.
Mkurugenzi huyo alisema takriban asilimia 80 ya nyama itafungashwa na kuuzwa nje ya nchi  hasa Uarabuni kwa sababu nyama ya mbuzi ya Tanzania imebainika kuwa na mvuto maalum katika nchi hizo.
“Mbali na uwekezaji huu wa kiwanda cha nyama pia tunatazamia kuwekeza katika mnyororo wa thamani kuanzia kusindika ngozi inayotoka kiwandani hadi kuzalisha viatu, mikanda na bidhaa zote za ngozi na kupunguza uagizaji wa bidhaa hizo kutoka nje ya nchi,” alisema.
Mrutu alisema nia yao ni kuitikia wito wa Rais Dk. John Magufuli wa kutaka viwanda vizalishe viatu nchini kuanzia vya majeshi na wananchi wote ambapo wamepanga kuanzia mwakani wataanza kuuza bidhaa hizo.
Aliongeza kuwa uwepo wa kiwanda hicho utatoa fursa kwa wafugaji na wakulima kuuza majani, mifugo na mazao ya chakula kama mtama, mahindi, ambapo tayari wameanza kuhamasisha jamii za wafugaji na wakulima wa Mvomero, Ngerengere na sehemu zinazozunguka eneo la kiwanda kuchangamkia fursa hiyo.
Katika hatua nyingine Waziri Mkuu ameuagiza uongozi wa wilaya ya Mvomero kufanya mapitio ya mashamba ili kujua wamiliki wake na kama hawajayaendeleza wachukue uamuzi wa haraka wa kuyatwaa na kuyarudisha mikononi mwa Serikali.
Waziri Mkuu alitoa agizo hilo wakati akijibu ujumbe uliokuwa katika mabango yaliyobebwa na wananchi wa kijiji cha Maji ya Chumvi wilayani Mvomero waliosimamisha msafara wakati ukitokea kwenye kiwanda cha nyama.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA