WAZIRI MWIGULU AFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA CHINA NCHINI TANZANIA


 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba(kushoto), akimsikiliza Balozi wa China nchini Tanzania Dkt. Lu Youqing (katikati), wakati wa mazungumzo juu ya  masuala ya ushirikiano katika sekta ya ulinzi na  usalama kati ya Tanzania na China, Kulia ni Msaidizi wa Balozi, Wang Fang. Mazungumzo hayo yalifanyika leo,jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba(katikati), akiangalia vipengele mbalimbali vinavyohusu ushirikiano juu ya masuala ya ulinzi na usalama, wakati wa mazungumzo yaliyomhusisha Balozi wa China nchini Tanzania, Dkt. Lu Youqing(kulia). Kushoto ni Mwakilishi Mkazi wa Jamhuri ya Watu wa China, Lin Zhiyong. Mazungumzo hayo yalifanyika leo,jijini Dar es Salaam.

Mwakilishi Mkazi wa Jamhuri ya Watu wa China, Lin Zhiyong(kulia), Msaidizi wa Balozi wa China nchini Tanzania, AI Zhuan(katikati) na Katibu wa Balozi, Dong Zhenyu(kushoto), wakimsikiliza Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba(hayupo pichani), wakati wa mazungumzo juu ya  masuala ya ushirikiano katika sekta ya ulinzi na  usalama kati ya Tanzania na China. Mazungumzo hayo yalifanyika leo, jijini Dar es Salaam.

 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba(katikati), akiagana na Mwakilishi Mkazi wa Jamhuri ya Watu wa China, Lin Zhiyong, mara baada ya kumaliza mazungumzo juu ya  masuala ya ushirikiano katika sekta ya ulinzi na  usalama kati ya Tanzania na China. Kulia ni Balozi wa China nchini Tanzania, Dkt. Lu Youqing. Mazungumzo hayo yalifanyika leo, jijini Dar es Salaam. (Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba(kushoto), akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa China nchini Tanzania, Dkt. Lu Youqing, mara baada ya kumaliza mazungumzo juu ya  masuala ya ushirikiano katika sekta ya ulinzi na  usalama kati ya Tanzania na China. Mazungumzo hayo yalifanyika leo, jijini Dar es Salaam.
IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI-WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*