WAZIRI NAPE APOKEA UWANJA WA TAIFA WA UHURU, "SHAMBA LA BIBI"




NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
SERIKALI imekabidhiwa rasmi uwanja wa Taifa wa Uhuru, (pichani juu), jijini Dar es Salaam, leo Agosti 22, 2016, baada ya ukarabati mkubwa wa uwanja huo kukamilika.
Akipokea uwanja huo kwa niaba ya Serikali, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, amewapongeza wakandarasi ambao ni kampuni ya China ya Beijing Construction Engineering Group Company Limited, (BCEG), na mshauri mwelekezi wa uwanja huo kampuni ya kizalendo chini ya uongozi wa ke, Injinia Aloyce Peter Mushi kwa kazi nzuri iliyofanyika licha ya mikwamo ya hapa na pale.

“Ndugu zetu Wachina, wameonyesha sio tu uhusiano mzuri bali wameonyesha kuwa wao ni ndugu zetu, kwani walishiriki wakati nchi yetu ikipata uhuru laini toka wakati huo hadi hivi sasa, bado wanashiriki katika kusaidia kuimarisha uchumi wetu,” alisema.
Waziri Nanuye aliwataka watumiaji wa uwanja huo kulipa ada za matumizi kama inavyostahili, ili hatimaye fedha hizo ziweze kugharimia matunzo ya uwanja.
Akitoa taarifa ya ujezni huo, mshauri huyo mwelekezi wa ujenzi, Injinia Aloyce Peter Mushi alisema, uwanja huo una uwezo wa kuchukua watu milioni 22 na ulikamilika na kuanza kutumika kwa mara ya kwanza Mei 22, 2015.
Naye Meneja Mkuu wa Kampuni ya BCAG, Cheng Long Hai, alisema, uwanja huo umewekewa mifumo yote muhimu kama vile tangi la kuhifadhia maji na mifumo ya maji taka, na kuishukuru serikaliya Tanzania kwa kuiaminikampuni yake kutekeleza mradi huo mkubwa.
Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Profesa Elisante Ole Gabriel, alisema, amekuwa akipokea maombi mbalimbali ya wanamichezo na watu wengine kuomba kuutumia uwanja huo na kuwahakikishia kuwa utaratibu unapangwa ili watanzania waanze kufaidi matunda ya uwanja huo ambao kutokana na ukongwe wake ulipachikwa jina la shamba la bibi.
“Nitoe rai tu kwa watanzania, leohii Agosti 22, 2016 ambapo tumekabidhiwa uwanja huu rasmi ukiwa umekamilika, naomba hilo jina la shambala bibi nalo lifikie kikomo kwani uwanja huu sa sa unauonekano mpya na wa kisasa.” Alisema Profesa Gabriel.
Ukarabati huo mkubwa ulihusisha ujenzi wa jukwaa na paa, ikiwa ni pamoja na miundombinu mingine ya uwanja kama vile, mifumo ya kusambaza maji, na kutoa maji taka, uwekani wa tanki la kuhifadhia maji, pamoja na ujenzi wa vyoo vya kutosha uwanjani.

 Waziri Nape akizungumza kabla ya kukabidhiwa uwanja huo Agosti 22, 2016. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Profesa Elisante Ole Gabriel, na kushoto ni mshauri wa ujenzi, Injinia Aloyce Peter Mushi (PICHA NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID)
 WaziriNape, (wapili kushoto), Katibu Mkuu Profesa Ole Gabriel, (wakwanza kushoto),
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Michezo, Alex Makoye Nkenyenge, (watatu kushoto) na Injinia Mushi, wakikagua uwanja huo
 Waziri Nape, akikagua nyasi bandia uwanjani
 Alama ya uwanja wa Uhuru ni jukwaa hili kuu, kama linavyoonekana leo Agosti 22, 2016
 Vyoo vya kisasa, (kushoto) wanawakena kulia wanaume

 Waziri akimpongeza Meneja wa Kampuni ya Kichina ya Beijing Construction Engineering Group Company Limited, (BCEG),
Cheng Long Hai
 Katibu Mkuu Profesa Ole Gabriel, (kulia) na Meneja Mkuu wa (BCEG),
Cheng Long Hai, wakisaini hati za makabidhiano ya uwanja mbele ya Waziri Nape
 Waziri Nape akishuhudia makabidhiano ya hati kuthibitisha sasa uwanja uko mikononimwa serikali
 Profesa Gabriel
 Injinia Mushi
 Cheng Long Hai
Waziri akizungumza jambo wakati wa ukaguzi wa nje wa uwanja huo

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI