WAZIRI WA MAMBO YA NDANI MWIGULU NCHEMBA AFANYA UKAGUZI KAMBI ZA WAKIMBIZI MKOANI KATAVI


Waziri wa Mambo ya Ndani nchini Mh.Mwigulu Nchemba leo amewasili mkoani Katavi,na kufanya ukaguzi kwenye kambi ya wakimbizi ya Katumba ambako kulikuwepo na zoezi la uhakiki wa waliokuwa wakimbizi kutokea kwa  majirani zetu Burundi na baadae kuamua kuwapa Uraia wa Tanzania mwaka 2009.Katika ukaguzi huo Mh.Mwigulu amesema kuwa zoezi la uhakiki linafanyika ili kuchunguza mienendo yao na uwepo wao kwenye eneo la Kambi,amesema kuwa kumekuwepo na taarifa za baadhi ya ndugu zetu ambao wamekuwa wakijihusisha na watu waovu,kufanya vitendo vya kibaguzi na kutoka nje ya kambi zao na kwenda nchi jirani bila kibali.
Mh.Mwigulu amesema kuwa mbali ya kambi ya Katumba,pia ametembelea kambi ya Mishamo na kuviagiza vyombo vya usalama na kupitia Seririkali za mitaa kuwachukulia hatua watu wanaojihusisha na vitendo hivyo,amaesema na kuongeza kuwa Tanzania haina tabia za kibaguzi"moja kati ya sifa kubwa ya nchi yetu ni kushinda vita dhidi ya ubaguzi wa aina yoyote tangu tulipopata uhuru" ,alisema Mh.Mwigulu.

"Natoa rai kwa raia wote tuliowapa kibali cha kufanya kazi,kuishi na kuwa raia wa nchi yetu, waache kujihusisha na vitendo viovu na vya kibaguzi.Hatutawavumilia watu ambao tumewakaribisha kwa nia njema hapa nchini na baadae wahatarishe usalama na amani ya nchi yetu",alisema Mh.Mwigulu.

Mwigulu alibainisha pia kuwa amekutana na Askari wa jeshi la polisi na idara zake zote na pia ametembelea gereza la mpanda ikiwa ni ziara ya kupata uhalisia wa changamoto zinazokabili jeshi la polisi,Magereza,Uhamiaji na zimamoto kwa kila mkoa,ambapo tayari kwa majawabu ya kudumu.













Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.