YANGA KWENDA LUBUMBASHI JUMAPILI KUKAMILISHA RATIBA KOMBE LA AFRIKA


Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
KIKOSI cha Yanga SC kitafanya mazoezi Ijumaa na Jumamosi kabla ya safari ya Lubumbashi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kwa ajili ya mchezo wa mwisho wa Kundi A Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya TP Mazembe Jumanne ijayo.
Wachezaji wa Yanga wamekuwa na mapumziko ya kutwa yote ya leo baada ya jana kufungwa kwa penalti 4-1 na Azam FC kufuatia sare ya 2-2 katika mchezo wa Ngao ya Jamii Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Na sasa wanajiandaa wa mchezo wa kukamilisha ratiba Kombe la Shirikisho wiki ijayo na wataondoka Dar es Salaam Jumapili.
Kikosi cha Yanga SC kilichifungwa na Azam FC jana Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam
Mchezo huo unatarajiwa kuchezeshwa na refa Helder Martins De Carvalho wa Angola, atakayesaidiwa na washika vibendera Jean Claude Birumushashu wa Burundi na Arsenio Chadreque Marengula wa Msumbiji.
Maofisa wengiene wa mchezo huo watakuwa ni Antonio Muachihuissa Caxala wa Angola, Gerges Rodolphe Bibi wa Shelisheli, Ali Mohamed Ahmed wa Somalia na Russell Paul wa Afrika Kusini.
Mazembe inaongoza Kundi A kwa pointi zake 10 baada ya mechi tano na imekwishafuzu Nusu Fainali, ikifuatiwa na Medeama yenye pointi nane, Mouloudia Olympique Bejaia pointi tano na Yanga inayoshika mkia kwa pointi zake nne. 
Medeama itahitaji hata sare Jumanne dhidi ya wenyeji Mouloudia Olympique Bejaia nchini Algeria ili kwenda Nusu Fainali. 
0

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MATOKEO YA KIDATO CHA PILI, DARASA LA SABA YATANGAZWA ZANZIBAR

HIVI NDIVYO BIASHARA YA NGONO NAMNA INAVYOTIKISA MOROGORO: SEHEMU YA PILI.

ZAIDI YA WANANCHI 500 KUSHIRIKI MAFUNZO YA MKIKITA YA KILIMO CHA PAPAI SALAMA

MKIKITA YATOA OFA KWA KILA HEKA YA PAPAI SH. MIL. 2 KUTANDAZA MIUNDOMBINU YA UMWAGILIAJI

DIAMOND AITWA NA NYOTA YAJAA GOMS

WATEJA WA NSSF DAR WATIMULIWA KWA MTUTU WA BUNDUKI

MATOKEO YA DARASA LA SABA YATANGAZWA

KAMISHNA MARIJANI AZINDUA CHAMA CHA WAFUGAJI MBWA TANZANIA (TCA)