SIMBA ILIVOIADHIBU POLISI DODOMA

Ligi Kuu soka Tanzania bara imesimama kwa baadhi ya michezo kuahirishwa kutokana na timu husika kutoa wachezaji wengi katika kikosi cha Taifa Stars kilichopo Nigeriakupambana na wenyeji wao katika mchezo wa kukamilisha ratiba ya michuano ya kuwania kufuzu AFCON 2017.
IMG_0082
Wakati baadhi ya michezo ya Ligi Kuu ikiendelea Simba ambao ni moja kati ya vilabu vilivyoahairishiwa michezo kutokana na kutoa wachezaji wake katika timu za taifa, imecheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Polisi Dodoma katika uwanja wa Jamhuri Dodoma, mchezo ambao ulihudhuriwa na wa naibu spika wa bunge DK Tulia Ackson na waziri wa mwenye dhamana ya michezo Nape Nnauye.
IMG_0101
Katika mchezo huo ambao ulihudhuriwa na mashabiki wengi wa Dodoma kutokana na kuwa na kiu ya kuzikosa Simba na Yanga zikija katika uwanja wao wa Jamhuri, mchezo ulimalizika kwa Simba kuwaadhibu Polisi Dodoma wanaoshiriki Ligi daraja la kwanza kwa goli 2-0, magoli ya Simba yalifungwa na Abdi Banda dakika za nyongeza kabla ya kwenda mapumziko na Saidi Ndemla dakika ya 60.
IMG_0054
Waziri Nape akiongea na afisa habari wa Simba Haji Manara
IMG_0049
Naibu Spika DK Tulia alipokuwa anawasili uwanjani

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI