HANS POPPE AMZAWADIA GARI NA MKWANJA TSHABALALA, ASEMA HAJIB LAKE LIPO NJIANI


Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
MWENYEKITI wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe amemzawadia gari aina ya Toyota Raum beki Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ kutokana na kazi yake nzuri kwa sasa katika klabu.
Kapteni huyo wa zamani wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), amemzawadia gari hilo Tshabalala asubuhi ya leo ofisini kwake, Mbezi Tangi Bovu, Dar es Salaam.
Na Hans Poppe akasema anaweza kutoa zawadi ya aina hiyo kwa mchezaji yeyote mwingine wa Simba SC atakayefuata nyayo za Tshabalala kwa kujituma na kuisaidia timu.
Hans Poppe (kulia) akimkabidhi kadi ya gari Tshabalala leo Dar es Salaam
Hapa Hans Poppe anamkabidhi Tshabalala fedha za mafuta kwa miezi sita

Poppe amesema zawadi hiyo iliyoambatana na fedha taslimu Sh. Milioni 1 ya mafuta kwa miezi sita, haimo kwenye vipengele vya Mkataba wake wa sasa unaomalizika mwishoni mwa msimu.
“Hiyo ipo nje ya Mkataba wake, nimempa zawadi tu kutokana na juhudi zake kwa sasa. Na nitatoa zawadi hiyo kwa yeyote ambaye atafuata nyayo zake. Na nadhani zawadi kama hii inanukia kwa Ibrahim Hajib,”amesema Poppe.
Tshabalala aliye katika msimu wake wa pili Simba SC tangu asajiliwe kutoka Kagera Sugar amekuwa mchezaji muhimu kwenye timu hiyo kwa sasa.
Pamoja na kufanya vizuri kazi yake ya ulini, lakini pia Tshabala amekuwa akihusika karibu katika kila bao la Simba, aidha kwa kutoa pasi ya moja kwa moja au kusaidia shambulizi la bao
0

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

NAMAINGO YAZINDUA HEKA 7000 ZA MASHAMBA MJI KIJIJI CHA MSOLWA, MKURANGA

HIVI NDIVYO BIASHARA YA NGONO NAMNA INAVYOTIKISA MOROGORO: SEHEMU YA PILI.

HABARI MPASUKOOO:GARI LAGONGA WATOTO KUIKWEPA BODABODA GONGO LA MBOTO

HARAMBEE YA UJENZI HOSPITALI YA MUHEZA YAVUKA MALENGO, ZAPATIKA BIL. 1.6

WAZIRI SHONZA AMJIBU DIAMOND

HABARI MPASUKOOO!!! MCHAWI ADONDOKA AKIWA UCHI KIVULE,DAR

WAPENZI WANASANA WAKIFANYA MAPENZI GESTI

DIAMOND AITWA NA NYOTA YAJAA GOMS