KFC YATOA MSAADA WA VIFAA VYA BRAILLE KWA WANAFUNZI WENYE ULEMAVU WA KUONA NA KUSIKIA KATIKA SHULE YA MSINGI UHURU MCHANGANYIKO JIJINI DAR.

KAMPUNI ya KFC Kuku Foods Limited Tanzania wametoa msaada wa 
vifaa vya braille kwa wanafunzi wenye ulemavu wa kuona na kusikia wa shule ya msingi Uhuru Mchanganyiko iliyopo kariakoo jijini Dar es Salaam.

Katika halfa ya makabidhiano ya vifaa maalum kwa Shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko iliopo Kariakoo, KFC Meneja Mkuu wa KFC Tanzania, Louis Venter
amesema kuwa vifaa hivyo vitawasaidia wanafunzi wenye mahitaji maalum ambao ni wasio na uwezo wa kuona na wale wasioweza kusikia Vile vile Msaada huo ni muundelezo wa ushirikiano na uhusiano wa karibu kati ya Kampuni ya KFC na Shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko. 

Meneja Mkuu wa KFC Tanzania Bwana Louis Venter amesema, “ Dhumuni la Mchango wetu ni kusaidia kuboresha mazingira ya kijamii ya watoto hawa. Tunataka mchango huu wa kampuni yetu uwe wa maandalizi ya uzinduzi wa programu maalum iitwayo ‘Add Hope Program’ ya kusaidia jamii nchini Tanzania mwezi Oktoba mwaka huu.”

Kampuni ya KFC imedhamiria kutoa msaada kwa shule hii yenye mahitaji maalum kwa kipindi endelevu.
Meneja Mkuu wa KFC Tanzania, Louis Venter akizungumza na wanafunzi wa shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko pamoja na wafanyakazi pamoja na walezi wa wanafunzi wenye ulemavu wanaosoma katika shule hiyo jijini Dar es Salaam na kutoa msaada wa vifaa vinavyowasaidia watoto wenye ulemavu wa macho(Upofu).
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko, Anna Mshana akizungumza mara baada ya kupokea msaada wa shule ya msingi Uhuru Mchanganyiko.
Mkuu wa Kitengo cha Wanafunzi Walemavu katika Shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko, Ahmed Abdallah akizungumza wakati wa kukabidhiwa vifaa vya braille kwa wanafunzi wenye ulemavu wa kuona na kusikia wa shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko iliyopo Kariakoo jijini Dar es Salaam.
Meneja Mkuu wa KFC Tanzania, Louis Venter akizungumza wakati wa kukabidhi wa vifaa vya braille kwa wanafunzi wenye ulemavu wa kuona na kusikia wa shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko iliyopo Kariakoo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Uhuru Mchanganyiko wenye ulemavu wa kuona na kusikia wakiwa katika hafla fupi ya kukabidhiwa vifaa vya braille ambavyo vitawasaidia katika masomo yao.
Baadhi ya wafanyakazi wa KFC watitoa msaada wa vifaa vya braille kwa wanafunzi wenye ulemavu wa kuona na kusikia kwa Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko, Anna Mshana jijini Dar es Salaam.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko, Anna Mshana akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa KFC jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Mkufunzi mmojawapo mwenye ulemavu wa kuona, Hadji Zuberi akiwashukuru waanyakazi wa KFC kwa kuona umhimu wa kutoa masaada katika shule ya Msingi Mchanganyiko iliyopo Kariakoo jijini Dar es Salaam leo.
0

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

HIVI NDIVYO BIASHARA YA NGONO NAMNA INAVYOTIKISA MOROGORO: SEHEMU YA PILI.

ANGALIA PICHA NDEGE KUBWA YA ABIRIA DUNIANI ILIYOANZA SAFARI NDEFU ZAIDI!

WAPENZI WANASANA WAKIFANYA MAPENZI GESTI

LICHA YA UZURI WAKE MWANADADA ELIZABETH MICHAEL a.k.a LULU SI MALI KITU MBELE YA RAY, AMKWEPA KUOGOPA AIBU.

IJUE HISTORIA YA UHASIMU WA KOREA KASKAZINI NA MAREKANI

NCHI YA URUSI NDIYO NCHI INAYOONGOZA KWA KUWA NA UBORA WA ELIMU NA VYUO DUNIANI.

YANGA SC WAANZA KAZI AFRIKA LEO…WANAKIPIGA NA U.S.M. ALGER SAA 4:00 USIKU ALGERIA

DC MJEMA AONJA ADHA YA MAFURIKO AKIKAGUA ATHARI ZA MAFURIKO ILALA

KWA HERI KAMANDA WETU ABBAS KANDORO