Wachezaji wa Kilimanjaro Queens wakiahangilia ubingwa wa Chalenji Cup kwa wananwake mjini Jinja leo baada ya kuibwaga timu ya Kenya.
Haikuwa ubashiri, badala yake ilikuwa ni mipango thabiti ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kuhakikisha kwamba inavuna ushindi na kuwa mabingwa wa Kombe la Chalenji la CECAFA kwa wanawake baada ya kuilaza Kenya mabao 2-1 katika mchezo wa fainali uliofanyika Uwanja wa Nambole jijini Jinja nchini Uganda.
Comments