MAFUNZO KUHUSU MWONGOZO WA USIMAMIZI WA UWEKEZAJI WA MIRADI YA UMMA KANDA YA MOROGORO YAFUNGULIWA RASMI


 Mgeni Rasmi, Bi. Lorah Madete, Kaimu Naibu Katibu Mtendaji, Klasta ya Uchumi Jumla, Tume ya Mipango, akitoa hotuba wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku tano kuhusu Usimamizi wa Uwekezaji wa Miradi ya Umma Kanda ya Morogoro kwa Maofisa na Watendaji wa Idara za Sera na Mipango. Waliokaa ni Bi. Anna Kimwela, Mchumi, Tume ya Mipango na Dr. Jehovaness Aikaeli, Mhadhiri Mwandamizi na Mkuu wa Idara ya Uchumi, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

 Washiriki wa Mafunzo kuhusu Mwongozo wa Usimamizi wa Uwekezaji wa Miradi ya Umma ambao ni Maofisa na Watendaji wa Idara za Sera na Mipango kutoka Kanda ya Morogoro wakimsikiliza Mgeni Rasmi (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo yanayofanyika katika Ukumbi wa Mkutano katika Chuo Kikuu cha Kilimo Morogroro (SUA). 

 Washiriki pamoja na wakufunzi wa mafunzo juu ya Mwongozo wa Usimamizi wa Uwekezaji wa Miradi ya Umma ambao ni Maofisa na watendaji wa Idara za Sera na Mipango kutoka Kanda ya Morogoro wakiwa katika picha ya pamoja na Mgeni Rasmi, Bi. Lorah Madete, Kaimu Naibu Katibu Mtendaji, Klasta ya Uchumi Jumla, Tume ya Mipango (aliyekaa wa pili kushoto) mara baada ya ufunguzi wa mafunzo hayo.
Muwezeshaji Dr. Jehovaness Aikaeli, Mhadhiri Mwandamizi na Mkuu wa Idara ya Uchumi, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akitoa elimu kwa washiriki wa mafunzo hayo.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA