MAMA LWAKATARE AWATOA WAFUNGWA 12 GEREZA LA KEKO


Mchungaji Kiongozi, Dk. Getrude Lwakatare,  kupitia kanisa lake la Assemblies  of God (Mlima wa Moto) aliwalipia wafungwa 78 katika magereza matatu ya jijini Dar  es Salaam na kuachiwa huru baada ya kulipa faini ya shilingi milioni 25 zilizochangwa na waumini wa kanisa hilo.
Shughuli hiyo ilifanyika jana chini ya kiongozi huyo wa kiroho ambaye alikuwa ameongozana na waumini wa kanisa lake walioanzia katika gereza la Keko na baadaye kuelekea Ukonga na Segerea.
mama-lwakatare-1
Mchungaji Kiongozi, Dk. Getrude Lwakatare wa kanisa la Assemblies of God (Mlima wa Moto) akizungumza na vyombo vya habari.
mama-lwakatare-2
…Akifafanua jambo kwa wanahabari.
mama-lwakatare-3
Wanahabari wakiendelea kuchukua tukio hilo.
mama-lwakatare-4
Baadhi ya waumini wa kanisa la Assemblies of God wakiongozana na Dk. Lwakatare baada ya kutoka Gereza la Keko kuelekea kwenye magari.
mama-lwakatare-5
Lwakatare akiendelea kufafanua mambo mbalimbali kwa wanahabari.
Katika siku ya jana aliwatoa wafungwa 50 na baadaye siku nyingine angelienda kuchukua 28 waliobaki kutokana na kuwepo kwa kasoro ndogondogo za kukosewa kwa majina yao.
Lwakatare baada ya kukabidhiwa wafungwa hao aliwapakia katika mabasi yake aliyokuwa ameyaandaa hadi katika kanisa lake lililopo Mikocheni B jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuwapa huduma ya kuoga, chakula na nguo mpya zilizokuwa zimenunuliwa na waumini wa kanisa hilo.
Akizungumza na wanahabari waliofika kwenye tukio hilo, Lwakatare alisema kuwa ametoa wafungwa 12 kwanza kutoka gereza la Keko na ameamua kufanya hivyo kutokana na fedha zilizochangwa na waumini wa kanisa lake walioguswa na roho mtakatifu ili wafungwa waliofungwa kwa makosa madogo waweze kurudi uraiani kwani wengine walifungwa kwa makosa ya kudaiwa kama kiasi cha shilingi milioni moja.
Aliongeza kwamba hawafahamu wafungwa aliowatoa bali ni Mungu ndiye aliyemwelekeza namna ya kusaidia watu wenye matatizo, huku akiamini  kwamba watu hao wakitoka na kuingia uraiani watakuwa watu wema.
Alifafanua kuwa wafungwa hao walihukumiwa vifungo kati ya miezi sita hadi miaka mitatu na walitakiwa kulipa faini ama kufungwa,  na kulingana na taratibu za kisheria anapolipa huachiliwa huru.
“Faini za wafungwa hao zilikuwa kati ya shilingi 50,000 hadi 500,000 na baada ya kuzikosa walitakiwa kupelekwa jela,” alisema Lwakatare na kuongeza kuwa baada ya taratibu zote kukamilika ikiwemo kuwapatia nguo na hata kuwalisha neno la Mungu atawapa nauli ili kila mmoja arudi kwao kwa ajili ya kuungana na familia yake.
Mwandishi wetu alipata nafasi ya kuzungumza na mmoja wa  wafungwa walioachiwa huru mmoja wao akiwa Hamis Abdallah ambaye alisema,
“Jamani mimi naitwa Hamis Abdallah, kwa kweli ninamshukuru sana Mama Lwakatare kwa kuona sisi ni watu muhimu na tunaohitaji kurudi kuangalia familia zetu  kama mimi niliyemwacha mke wangu akiwa na mtoto mchanga na nilifungwa kwa kukosa kulipa faini ya Sh.300,000 kutokana na kosa ambalo siwezi kukutajia.”
Na Denis Mtima/GPL
0

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

HIVI NDIVYO BIASHARA YA NGONO NAMNA INAVYOTIKISA MOROGORO: SEHEMU YA PILI.

WAPENZI WANASANA WAKIFANYA MAPENZI GESTI

LICHA YA UZURI WAKE MWANADADA ELIZABETH MICHAEL a.k.a LULU SI MALI KITU MBELE YA RAY, AMKWEPA KUOGOPA AIBU.

ANGALIA PICHA NDEGE KUBWA YA ABIRIA DUNIANI ILIYOANZA SAFARI NDEFU ZAIDI!

IJUE HISTORIA YA UHASIMU WA KOREA KASKAZINI NA MAREKANI

MATOKEO YA DARASA LA SABA YATANGAZWA

ZIARA YA KATIBU MKUU WA CCM NDUGU KINANA NDANI YA CHAKE CHAKE,MKOA WA KUSINI PEMBA LEO.

NCHI YA URUSI NDIYO NCHI INAYOONGOZA KWA KUWA NA UBORA WA ELIMU NA VYUO DUNIANI.