PAPA FRANCIS AKUTANA NA RAIS KABILA



Papa Francis akiagana na Rais Kabila baada ya mazungumzo kumalizika.
VATICAN CITY: Papa Francis amekutana na kufanya mazungumzo ya faragha na Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Mazungumzo hayo yalifanyika kwenye makazi ya Papa Francis yaliyoko jijini Vatican.
Kwenye mazungumzo hayo Rais Kabila amesema atahakikisha anafanikisha mazungumzo ya pande zote zinazokinzana nchini Congo yamalizike kwa amani.
Kwenye mazungumzo hayo yaliyochukua dakika 20, Papa Francis hakwenda kusalimiana na mgeni wake huyo kwenye chumba maalum cha wageni maalum na kumsubiri kwenye maktaba yake.
Vatican wamesema Papa Francis amesisitiza ni lazima mazungumzo ya amani yafanyike baina ya serikali na wapinzani ili kuliepusha taifa hilo kuingia kwenye machafuko.
Na Leonard Msigwa/GPL.
 Papa Francis akiagana na Rais Kabila baada ya mazungumzo kumalizika.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI