Penzi La Wakongo Lamaliza Mastaa Bongo!


wolper-21Staa wa sinema za Kibongo, Jacqueline Wolper akiwa  na aliyekuwa mpenzi wake Mkongo.
Na Hamida Hassan, Uwazi.
Imefichuka kuwa, baadhi ya wanaume kutoka Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo (DRC) waliopiga makazi yao Bongo, wamewamaliza mastaa nchini kutokana na penzi la pesa wanalolimwaga kwao, Uwazi limechimba. 
Kwa mujibu wa chanzo cha karibu na mastaa waliokwishagawa penzi kwa Wakongo hao, kinachoonekana sasa ni mashindano ya mastaa wa Bongo kila mmoja kwa nafasi yake kuhakikisha anafaidi pesa za mapedeshee hao licha ya kwamba, mapenzi yao hayadumu. “Jamani nyie watu wa Global, sidhani kama mmewahi kufanya uchunguzi wa kina na kubaini kuhusu hawa wanaume wa kutoka Kongo. Baadhi yao wamekuwa wakigawa pesa ili kuwapata mastaa wa Bongo.
2Staa wa Bongo Movies, Wema Sepetu akiwa na Mkongo.
“Ndiyo maama ukifuatilia utagundua kuwa, kila kukicha, Mkongo f’lani kamchukua staa f’lani. Mbaya zaidi, mastaa wanazungukana wenyewe kwa wenyewe. Leo utasikia Mkongo yupo na huyu, kesho yupo na yule na wenyewe mastaa wanajua, lakini hawakatai maana wao wanataka pesa tu,” alisema mtoa habari huyo ambaye naye ni staa lakini asiyetaka ‘kujinajisi’ na jasho la Wakongo hao. Mnyetishaji huyo aliendelea kuweka wazi kwamba, maisha ya Wakongo hao hapa Bongo ni ya taiming:
13562063_1044944048916110_1041740578_n
   Mwanamitindo Bongo, Hamisa Mobeto.
“Kuna wakati wanachacha sana. Lakini wakipata ndiyo kufuru yao inakuwa kwa wenzangu na mimi. Mimi aka! N’takula pesa za mwanaume mwenye mapenzi na mimi lakini siyo wanaofuata majina makubwa kama fasheni. Nyie fuatilieni mtagundua mastaa walionasa kwa Wakongo wote wana majina makubwa, sasa hapo amebaki nani?
 “Halafu hawa jamaa, pesa nyingi wanazipata kutoka kwenye nchi za Ufaransa, Ubelgiji na Dubai. Sijui kule wanafanya dili gani? Ila akitokea amekwenda kule akiwa mchovu, akirudi hatulali mjini. Kwa kweli pesa ni za kumwaga kwani katika hali halisi, wanaume hao wanawazidi wa Kitanzania kwa kuhonga. “Wapo mastaa wanahongwa shilingi milioni ishirini mpaka hamsini. Ndiyo maana unawaona mastaa wenzangu wengine hawachezi filamu muda mrefu, lakini wanaishi sawa, wanakula, wanavaa, wanakwenda saluni, wana magari, wanaweka mafuta na wanafanya bethidei tena za kufuru.”
shamsa89
Staa wa Bongo MoviesShamsa Ford. 
KUMBUKUMBU YA UWAZI 
Kumbukumbu ya gazeti hili, mpaka sasa, mastaa wa Bongo ambao wameshaandikwa kwenye magazeti pendwa kuwa wanatoka au wamewahi kutoka na wanaume Wakongo ni kama ifuatavyo: Wema Sepetu na Husna Idi, wao wameshaandikwa kutoka na Mkongo aitwaye Mwami Rajab ambapo siku za karibuni, mkewe wa Mwami, Nora Chilu alijitokeza na kuwapiga mkwara mastaa hao kuachana na mumewe.
 Jacqueline Wolper, yeye amewahi kuandikwa kutoka na Mwami, lakini baadaye wakamwagana na kunasa kwa Mkongo mwingine, Putin ila kwa sasa wememwagana. Hivi karibuni, mwigizaji mwingine Bongo, Shamsa Ford  ambaye kwa sasa ni mke wa mtu, aliandikwa akidai kuwa, Mkongo wa Wolper na Wema (hakumtaja jina) amemtongoza lakini akamchomolea mbali. 
97d6b53ace02e8f9e0bd2b084f27e90fMwanamuziki na Mwigizaji wa filamu za Bongo, Baby Joseph Madaha ‘Baby Madaha.
Pia, mwanamitindo mwenye mvuto Bongo, Hamisa Mobeto amewahi kuandikwa kunasa mtungo wa Mkongo, Mwami. Mobeto alibainika baada ya meseji zake za simu kunaswa akiomba pesa za kulipia mapazia. Staa mwingine aliyewahi kuandikwa kutoka na Mkongo huyo ni Video Queen wa Bongo, Agnes Gerald ‘Masogange’.
agnes-gerald-masogangeVideo Queen wa Bongo, Agnes Gerald ‘Masogange’.
Pia, aliyewahi kushiriki Bongo Star Search, Baby Joseph Madaha, hivi karibuni aliandikwa kumzoa bwana wa Wema ambaye ni Mkongo aliyejulikana kwa jina la John na walilala wote hotelini nchi jirani. 
Kuhusu msanii Elizabeth Michael ‘Lulu’ yeye aliwahi kuandikwa na Mkongo, Mwami. Mkongo huyo alisema anamtaka msanii huyo kwa gharama yoyote ile. Lakini siku chache, Lulu alijibu kuwa, kama Mkongo huyo angekuwa na mapenzi ya kweli asingeyaeleza kwenye magazeti.
0

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

HIVI NDIVYO BIASHARA YA NGONO NAMNA INAVYOTIKISA MOROGORO: SEHEMU YA PILI.

DC MJEMA AONJA ADHA YA MAFURIKO AKIKAGUA ATHARI ZA MAFURIKO ILALA

DC MKURANGA AZINDUA MRADI WA MASHAMBA MJI YA NAMAINGO MSOLWA

ANGALIA PICHA NDEGE KUBWA YA ABIRIA DUNIANI ILIYOANZA SAFARI NDEFU ZAIDI!

TGGA WAMUAGA BOSS WA GIRL GUIDES AFRIKA KWA HAFLA KABAMBE

WAPENZI WANASANA WAKIFANYA MAPENZI GESTI

IJUE HISTORIA YA UHASIMU WA KOREA KASKAZINI NA MAREKANI

Wasafi TV kuanza kurusha matangazo yake leo (+video)

WAGGGS AFRIKA WAIPONGEZA TGGA KWA KUONGOZA AFRIKA KUSAJILI GIRL GUIDES WENGI