RAIS MAGUFULI AZIDI KUPONGEZWA


 
Mwenyekiti wa Taasisi inayoshughulikia masuala ya Afrika (Africa Matters Limited) Mhe. (Baroness) Lynda Chalker wa Wallasey - Uingereza, amempongeza Rais wa Tanzania Dkt. John Magufuli kwa kupiga vita rushwa na kujenga mazingira bora kwa wekezaji.
Mhe. Lynda Chalker ametoa pongezi hizo leo tarehe 31 Agosti, 2016 Ikulu Jijini Dar es Salaam alipokutana na kufanya mazungumzo na Rais Magufuli kuhusu masuala mbalimbali ikiwemo hali ya uwekezaji hapa nchini.
"Mhe Rais amefanya uamuzi sahihi wa kupiga vita rushwa na kuiweka nchi hii katika njia mpya ya uwekezaji mzuri na hicho ndicho tumekuwa tukikizungumza, nimejitahidi kutoa ushauri wangu wa namna mimi na kampuni yangu binafsi tunaweza kumsaidia, nionavyo mambo yanakwenda katika mwelekeo mzuri" Amesema Mhe. Lynda Chalker.
Kwa Upande wake Rais Magufuli amemshukuru Mhe. Lynda Chalker kwa ushauri na dhamira yake ya kutaka Tanzania ipige hatua kimaendeleo na amemuomba kutumia ushawishi wake kuwahamasisha wawekezaji mbalimbali kutoka nchini Uingereza na kwingineko duniani kuja kuwekeza nchini Tanzania ili kuharakisha zaidi maendeleo.
Hata hivyo Dkt. Magufuli amesema wawekezaji wanaokuja Tanzania hawana budi kuwa wawekezaji makini.
"Ninawakaribisha wawekezaji makini kutoka Uingereza na mahali popote duniani, lakini nisingependa kupata wawekezaji wababaishaji" Amesisitiza Rais Magufuli.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.