RAIS MAGUFULI KUZINDUA NDEGE MPYA LEO


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli leo  anatarajiwa kuzindua ndege mbili mpya aina ya Bombardier Q 400 zilizonunuliwa na Serikali hivi karibuni.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi) Dkt. Leornard Chamuriho amesema maandalizi yote kwa ajili ya uzinduzi wa ndege hizo yamekamilika na uzinduzi huo utafanyika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) kuanzia saa mbili asubuhi.

“Tunawaomba wanahabari na wananchi kujitokeza kwa wingi katika uzinduzi huo ili waone utekelezaji wa ahadi wa Serikali katika mkakati wa kuhuisha usafiri wa Anga hapa nchini”, amesema Dkt. Chamuriho.
Ndege hizo aina ya Bombardier Q 400 zenye uwezo wa kubeba abiria 76 kila moja zimetengenezwa nchini Canada na zitahudumia soko la ndani ndani na nchi za jirani zitakapoanza kazi

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI