TAMBWE, NGOMA WAMNYAMAZISHA JULIO KAMBARAGE, YANGA YAILAZA MWADUI 2-0


Na Mwandishi Wetu, SHINYANGA
YANGA SC imeendeleza wimbi la ushindi katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya kuilaza Mwadui FC 2-0 Uwanja wa Kambarage, Shinyanga.
Shukrani kwao wafungaji wa mabao hayo, Mrundi Amissi Tambwe kipindi cha kwanza na Mzimbabwe Donald Ngoma kipindi cha pili. 
Mfungaji bora wa Ligi Kuu, Tambwe alifunga bao la kwanza dakika ya tano kabla ya Ngoma kufunga la pili dakika ya 90 na ushei.
Na kwa matokeo hayo, Yanga SC inafikisha pointi 10 baada ya mechi nne, ikishinda tatu na kutoa sare moja ikipanda hadi nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu. 
Amissi Tambwe (kushoto) na Donald Ngoma (kulia) wakishangilia baada ya kufunga leo Uwanja wa Kambarage
Donald Ngoma akimtoka beki wa Mwadui leo Uwanja wa Kambarage

Simba SC yenye pointi 13 za mechi tano inaongoza Ligi Kuu, wakati Azam FC yenye pointi 10 sawa na Yanga ni ya tatu kwa kuzidiwa wastani wa mabao.
Matokeo ya mechi nyingine za Ligi Kuu leo, Mbao FC imepata ushindi wa kwanza baada ya kuifumua Ruvu Shooting 4-1 Uwanja wa Mabatini, Mlandizi, Pwani, Ndanda FC wameshinda 2-1 dhidi ya wenyeji Maji Maji Uwanja wa Maji Maji, Songea na Mtibwa Sugar wameshinda 2-0 dhidi ya Kagera Sugar wakati Mbeya City imetoka sare ya 0-0 na Prisons Uwanja wa Sokoine, Mbeya.
Ligi Kuu inatarajiwa kuendelea kesho kwa mchezo kati ya Stand United na JKT Ruvu Uwanja wa Kambarage, Shinyanga wakati Jumanne African Lyon wataikaribisha Toto Africans ya Mwanza.
Kikosi cha Mwadui kilikuwa; Lucheke Mussa, Nassor Masoud ‘Chollo’, Yassin Mustapha, Iddy Mobby, Zahoro Jailan, Hassan Kabunda, Moris Kaniki, Paul Nonga, Rashid Ismail na Miraji Athumani
Yanga SC;Ally Mustafa ‘Barthez’, Juma Abdul, Mwinyi Hajji, Andrew Vicent, Kevin Yondan/Nadir Haroub 'Cannavaro', Mbuyu Twite, Simon Msuva, Thabani Kamussoko/Haruna Niyonzima, Amissi Tambwe, Donald Ngoma na Deus Kaseke/Juma Mahadhi.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*