BABU WA SAMUNGE AMZUIA MKUU WA MKOA WA ARUSHA



Wananchi wa Kijiji cha Samunge, Tarafa ya Sale, Wilayani Ngorogongoro wakiwa wamefunga barabara kuzuia msafara wa Mkuu wa Mkoa ili waweze kutatuliwa mgogoro ardhi ya Shule ya Msingi pamoja na Zahanati ya Samunge iliyoporwa na wavamizi. 
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo(tatu kulia) akisikiliza mgogoro wa wananchi wa Samunge baada ya wananchi hao kuzuia msafara wake. 
Mtendaji wa Kata ya Samunge Zacharia Antony (aliyeshika file) akimuonyesha Mkuu wa Mkoa Mhe. Mrisho Gambo(tatu kulia) barua iliyoandikiwa kinyume cha taratibu na Mkuu wa Kituo cha Polisi Loliondo kumhalalisha mvamizi katika eneo hilo na kuwaamuru wanakijiji kuacha kutombughudi Lemindi Njuda (Mvamizi). 
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo akienda kukagua eneo la shule ya Msingi Samunge lililovamiwa na Bw. Lemind Njuda (hayupo pichani). 
Mkuu wa Mkoa wa Arusha (pili kushoto) akionyeshwa mipaka ya eneo la Shule ya Msingi Samunge na viongozi wa kijiji cha Samunge. 
Wadau wa Habari katika picha ya pamoja na Babu wa Samunge Mchungaji Ambilikile Mwasapila(pili kulia) maarufu kama Babu wa Kikombe. 
Babu wa Samunge Mch. Ambilikile Mwasapila (kushoto) akiwa na Nteghenjwa Hosseah mdau wa Habari. Babu wa Samunge ni miongoni mwa wananchi waliozuia Msafara wa Mkuu wa Mkoa. 

…………………………………………………………. 

Nteghenjwa Hosseah ,Loliondo 

Migogoro ya ardhi katika wilaya ya Ngorongoro Mkoani Arusha juzi iliingia katika sura mpya baada ya wananchi wa kata ya Samunge wilayani humo akiwemo babu wa kikombe cha dawa, Mchungaji Ambilikile Mwaisapile waliandamana na kufunga barabara na kuzuia msafara wa Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo ili watatuliwe mgogoro wa ardhi ya shule iliyoporwa na diwani mstaafu wa kata hiyo. 

Wananchi hao wakiwa na mabango na majani mabichi walizuia msafara huo ili waweze kusikililizwa kilio chao cha muda mrefu baada ya baraza la kata kuamuru katika kesi yake aprill mwaka huu kuwa ardhi hiyo ni mali ya shule lakini jeshi la polisi Ngorongoro limekuwa likimlinda na kumkingia kifua mvamizi huyo na kukataa kutekeleza amri ya baraza la ardhi kata iliyomtaka kuondoka katika eneo hilo la shule. 

Baadhi ya mabango hayo yalikuwa yakisomeka ” tumeporwa ardhi yetu Mkuu wa Mkoa tusaidie” lingine likisema ”wenye fedha wamepora ardhi ya shule na polisi inawalinda na kuwakingia kifua” na bango lingine lililosomeka ”Mkuu wa Mkoa tunaomba ushuke utusikilize viongozi wa wilaya wote wamenunuliwa” 

Kabla ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha kuteremka kuwasikiliza aliteremka Mkuu wa wilaya ya Ngorongoro Rashid Taka na Mkuu wa polisi wa wilaya hiyo OCD Warioba kwa lengo la kuwatuliza na kuwasihii kuacha mukari ili waeleza kero zao kwa utulivu na amani bila ya vurugu zozote. 

Akizungumza kwa niaba ya wananchi wa kata hiyo, Mtendaji wa kata hiyo Zakaria Antony alisema kuwa eneo hilo lenye ukubwa wa ekari 15 limeporwa na mfanyabiashara na diwani mstaafu Lemindi Njuda ambaye amefanya kilimo cha migomba na shughuli nyingine za kijamii. 

Antony alisema kuwa uamuzi wa kuondolewa kwa diwani huyo wa zamani katika eneo la shule ulitolewa na baraza la ardhi kata aprill mwaka huu lakini jeshi la polisi wilaya ya Ngorongoro limekuwa likimlinda na kugoma kutekeleza amri baraza na badala yake limeandika barua ya kutobugudhiwa katika shamba hilo na hatua kali zinachukuliwa kwa mwananchi atayekiuka amri hiyo. 

Mtendaji huyo aliendelea kusema kuwa wananchi wanashindwa kufanya shughuli za maendeleo hususani ujenzi wa madarasa na nyumba za walimu kutokana na ufinyu wa eneo la shule hivyo walimuomba Mkuu wa Mkoa kusaidia mgogoro huo ili haki iweze kutendeka kwani polisi imewekwa mfukoni na tajiri huyo. 

Naye Mchungaji Ambilikile Mwaisapile alisema kuwa yeye yuko mstari wa mbele kuhakikisha shule inarudishiwa eneo lake lililoporwa na watu wenye fedha na nguvu za ushawishi kwani mungu hapendi vitu vya dhuruma. 

Mchungaji alisema yeye pamoja na wananchi wa kata hiyo walikuwa wakisaka haki kila ofisi ya wilaya ya Ngorongoro lakini haki hiyo walishindwa kuipata kutokana na mapokezi mabovu ya viongozi wa serikari wilaya ya Ngorongoro. 

Mkuu wa Mkoa Gambo kwa alimwamurisha OCD kufuta nakala ya barua aliyoandika mkuu wake wa kituo cha polisi Loliondo kwani yeye hana mamlaka ya kufanya hivyo bali anapaswa kutekeleza amri ya mahakama ya baraza la kata na sio vinginevyo. 

Gambo pia alimwagiza Mkuu wa wilaya ya Ngorongoro pamoja na kamati yake ya ulinzi na usalama kuhakikisha wanasimamia kikamilifu utekelezaji wa amri hiyo ili shughuli za maendeleo ya shule hiyo ziweze kufanyika mara moja. 

Alisema na kusikitishwa kuona wananchi wana kero ya kutaka maendeleo lakini viongozi wa serikali kwa kujali matumbo yao na kuendekeza rushwa wako mstari wa mbele kuzuia wananchi kufanya shughuli za ujenzi wa shule. 

Pia Mkuu huyo aliwataka viongozi wa wilaya kumaliza mgogoro mwingine wa ardhi uliopo karibu na zahanati ya kata hiyo ili wananchi waweze kufanya shughuli nyingine za maendeleo na kuacha kukesha kufikiria migogoro ya ardhi kila kukicha ambayo mingi inasababishwa na viongozi. 

Baada ya maelezo hayo wananchi walionyeshwa kufurahishwa na uamuzi huo na kuahidi kutoa ushirikiano wa hali na mali katika shughuli za maendeleo.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA