HABARI MPASUKOOO;Rais Magufuli afanya ziara ya kushtukiza Wizara ya Maliasili na Utalii

 Rais Dkt John Pombe Magufuli akikagua pembe za ndovu 50 zilizokamatwa katika operesheni maalum ya kusaka majangili alipofanya ziara ya kushtukiza makao makuu ya Wizara ya Maliasili na Utalii (MPINGO HOUSE) jijini Dar es salaam leo Oktoba 29, 2016
Rais Dkt John Pombe Magufuli akimpongeza kwa kazi nzuri Katibu Mkuu wa  Wizara ya Maliasili na Utalii Meja Jenerali Gaudence Milanzi baada ya kukagua akikagua pembe za ndovu 50 zilizokamatwa katika operesheni maalum ya  ya kusaka majangili alipofanya ziara ya kushtukiza makao makuu ya Wizara ya Maliasili na Utalii (MPINGO HOUSE) jijini Dar es salaam leo Oktoba 29, 2016o
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
Description: Description: Description: Description: Description: Coat of ArmsKURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU
Simu: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: press@ikulu.go.tz
Tovuti : www.ikulu.go.tz              
Faksi: 255-22-2113425

OFISI YA RAIS,
      IKULU,
 1 BARABARA YA BARACK OBAMA,  
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 29 Oktoba, 2016 amefanya ziara ya kushtukiza katika Ofisi za Wizara ya Maliasili na Utalii (Mpingo House) kwa lengo la kufuatilia utekelezaji wa operesheni ya kukabiliana na ujangili inayofanywa na Kikosi Kazi kilichoundwa na Wizara hiyo.
Akiwa katika ofisi hizo Rais Magufuli aliyekuwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Meja Jenerali Gaudensi Milanzi ameshuhudia pembe 50 za ndovu zilizokamatwa kati ya jana Ijumaa na leo Jumamosi Jijini Dar es Salaam.
Aidha, Dkt. Magufuli ameoneshwa magari yaliyokamatwa yakiwa yamebeba pembe hizo na watuhumiwa wanane wanaodaiwa kujihusisha na mtandao wa biashara haramu ya pembe za ndovu.
Rais Magufuli amewapongeza askari wote waliopo katika Kikosi Kazi cha kudhibiti na kupambana na biashara haramu ya pembe za ndovu pamoja na Raia wema wote wanaotoa ushirikiano katika operesheni hiyo na amewahakikishia kuwa anatambua kazi kubwa wanayoifanya na anawaunga mkono.
“Nawapongeza sana kwa kazi nzuri mnayoifanya na ninawahakikishia kuwa ninawaunga mkono, chapeni kazi, wakamateni wote wanaojihusisha na biashara hii haramu, hakuna wa kumbakiza, awe mkubwa au nani, kamateni, wala msijali cheo chake, umri wake, dini yake, kabila lake, umaarufu wake, sheria ni msumeno, watafuteni wote mpaka watu wakiona tembo wawe wanakimbia wenyewe ili tuokoe wanyama wetu ambao wanaendelea kutekelezwa.
“Hapa mmekamata pembe 50 maana yake tembo 25 wameuwawa, haiwezekani maliasili yetu ikawa inapotea hovyo hovyo kwa sababu ya watu wachache wenye tamaa ya kutaka utajiri wa haraka haraka” amesisitiza Rais Magufuli.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
2

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*