Mama wajawazito waaswa kuhusu ulaji wa matunda na mboga za majani

Na Mwandishi Wetu

Asilimia kubwa ya wanawake walio katika hali ya kupata ujauzito nchini wanakabiliwa na hatari ya kujifungua watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi kutokana na tabia ya kutopenda kula matudda na mboga za majani hivyo kukosa virutubsho muhimu mwilini.

Dk Hamis Shaabani daktari bingwa wa upasuaji wa mishipa ya fahamu  kutoka Taasisi ya mifupa(MOI) ameyasema hayo wakati wa zoezi la ufungaji upasuaji wa vichwa vikubwa na migongo wazi katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kigoma
Bi Anastazia Mtilili mkazi wa kijiji minyinga wilayani Kibondo akimuangalia binti yake Tedia Mwesiga baada ya kufanyiwa upasuaji wa kichwa kikubwa katila hospital ya rufaa ya Kigoma na madaktari toka MOI chini ya ufadhili wa GSM Foundation.

Dk Hamis alisema kuwa utafiti uliofanywa na Taasisi ya MOI mwaka 2002 unaonyesha zaidi ya watoto 4800 huzaliwa kila mwaka wakiwa na maradhi ya vichwa vikubwa na migongo wazi na kati yao 500 pekee ndiyo wanaoweza kufika hospital na kupatiwa matibabu.

Akizungumzia chimbuko la maradhi hayo Dk Hamisi alisema kuwa watoto wenye vichwa vikubwa na migongo wazi wanaweza kuzaliwa nacho au kupata siku chache baada ya kuzaliwa.

"Kwa wale wanaozaliwa na maradhi hayo ni kwasababu ya upungufu wa virutubisho ambavyo mama mjamzito anatakiwa avipate kabla ya kushika mimba  virutubisho hivyo vinapatikana  kwenye matunda, mboga za majani, mayai na vyakula vyote vyenye protini, pia maradhi ya mgongo wazi husababisha watoto kupooza na kushindwa kutumia miguu yao"alisema
Daktari bingwa wa upasuaji wa mishipa ya fahamu na ubongo kutoka MOI Dkt Khamis Shaabani (wa katikati)akimpa maelezo ya mtoto aliyefanyiwa upasuaji wa kichwa kikubwa Kaimu Katibu tawala wa Mkoa wa Kigoma Samweli Mtenga.

Alisema mpaka sasa kwa Mkoa wa Kigoma jumla ya watoto 48 walihudhuria kliniki na  wameshawafanyia upasuaji jumla ya  watoto nane wenye vichwa vikubwa sita na wawili wa mgongo wazi.

Ofisa habari wa GSM Foundation Khalfani Kiwamba alisema kuwa taasisi yao iliamua kudhamini matibabu ya maradhi ya vichwa vikubwa na migongo wazi baada ya kuelezwa changamoto mbalimbali za matibabu ya maradhi hayo na uongozi wa Taasisi ya MOI.

Anastazia Mtilili mkazi wa kijiji cha Minyinya Wilaya ya Kibondo akiongea kwa niaba ya wazazi ambao watoto wao wamefanyiwa upasuaji wa maradhi ya vichwa vikubwa na mgongo wazi aliwashukuru timu nzima ya madaktari hao pamoja na Taasisi ya GSM kwa msaada huo wa matibabu waliowapatia wa watoto wao bure.

Aliiomba jamii kuacha kuhusisha maradhi hayo na mila potofu za imani za kishirikina au mikosi kwenye familia hali inayofanya akina mama au baba kutelekezewa watoto.

Aliwaomba pia wataalam hao wasogeze huduma hiyo karibu na jamii hasa maeneo ya vijijini ambapo wapo watoto wengi wenye maradhi hayo wanateseka na hawana msaada.

"Nawaomba wazazi wenzangu hasa akinamama sababu sisi ndiyo tunakaa na watoto kwa muda mrefu ndiyo tunaoweza kugundua mabadiliko ya mtoto pia tusisikilize maneno ya dhihaka ya watu wa pembeni maradha haya yanatibika kabisa"alisema mzazi huyo
Mganga Mfawidhi wa hospital ya rufaa ya Kigoma(maweni)Dkt Fadhil Kibaya(wa katikati)akitoa maelezo mafupi kwa Kaimu katibu tawala wa Mkoa wa Kigoma Samwek Mtenga juu ya upasuaji uliofanyika kwa watoto wenye vichwa vikubwa na migongo wazi. 

Kaimu Katibu tawala wa Mkoa wa Kigoma Samwel Mtenga  aliwashukuru madaktari pamoja na shirika la GSM Foundation kwa udhamini huo wa matibabu bure kwa watoto wenye vichwa vikubwa na migongo wazi.

"Nawapongeza timu nzima ya GSM Foundation kwa uamuzi wenu huu wa kuja kuwapatia huduma hii ya upasuaji watoto wenye vichwa vikubwa na migongo wazi,Mkoa wetu upo pembezoni wazazi wengi wanashindwa kupeleka watoto wao muhimbili au Bugando kwasababu ya umbali na gharama"alisema

Pia aliwataka wazazi wenye watoto wenye maradhi hayo wasione aibu kuwapeleka hospitali ili waweze kupatiwa matibabu bure.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.