MATOKEO YA DARASA LA SABA 2016 SHULE YA SOUTHERN HIGHLANDS MAFINGA YAJIPONGEZA KUFANYA VIZURI


 Mwanafunzi  aliyeongoza masomo yote Rahma Mdeka akipokea cheti cha kuhitimu darasa la  saba na zawadi yake  wakati wa mahafali ya  shule ya  Southern Highlands Mafinga
 mkur
 Mkurugenzi wa shule za Southern Highlands Mafinga ,Mary  Mungai  kulia akitambulisha watumishi  wa  shule  hiyo.
 .........................................................................................................
Na MatukiodaimaBlog
 UONGOZI  wa  shule ya  Southern Highlands Mafinga wilaya ya  Mufindi mkoani  umeeleza kufurahishwa na matokeo ya mtihani wa darasa la  saba Taifa baada ya wanafunzi wote 51 waliofanya mtihani  huo kufaulu na kuifanya shule   hiyo kushika nafasi ya kwanza Kiwilaya .
 Pamoja na   kuongoza  kiwilaya  pia  shule   hiyo ya Southern Highlands Mafinga imekuwa shule ya 6 kati ya shule 232 katika  mkoa  wa Iringa na shule ya 198 kati  ya shule 8109 kitaifa .

Mkurugenzi mtendaji  wa  shule hiyo Mary Mungai akizungumza leo kufuatia matokeo hayo alisema  kuwa pamoja na  kuwa  shule  hiyo haijapata  kufelisha mwanafunzi hata  mmoja  toka  ilipoanzishwa 2001 ila bado ana imani  jitihada  zaidi  zitaongezwa  ili kuzidi kushika nafasi za juu zaidi  kimkoa na  kitaifa .
“   Ni jambo la kumshukuru Mungu na tunaendelea kumshukuru Yeye Kwa kuwezesha watoto wetu wa Southern Highlands School, kufaulu vizuri, kwa kishindo  kila mwaka wanafunzi wote  wamekuwa wakifaulu mitihani ya kitaifa ya darasa la saba na wote kuchaguliwa na kuendelea na masomo ya Sekondari....ni matumaini yetu imani kwa wazazi inazidi kuongezeka  zaidi kwa  shule yetu"
 

Alisema  kuwa  toka  shule  hiyo  ilipoanzishwa mwaka 1994 kama Day Care na Pre-school na mwaka 1997 kuanza shule ya msingi imekuwa ikifanya  vizuri na hakuna mtoto aliyepata  kufeli .
 

“Shule  yetu mwaka 2001 shule ilitoa wanafunzi wa kwanza wa darasa la Saba na wanafunzi walikuwa 17, wote walifaulu vizuri na wote walichaguliwa kuendelea na masomo ya kidato cha kwanza” 
Alisema katika  matokeo ya mitihani ya darasa la 7 ya mwaka 2001 Southern Highlands School ilishika nafasi ya kwanza kitaifa katika mitihani ya Somo la Kiingereza.
 Aidha  alisema  kwa  mwaka huu 2016 jumla ya wanafunzi 51 walisajiliwa  kufanya mtihani wa  darasa la  saba na  wote  walifanya wastani wa  shule 185.3137 kundi  la shule  watahiniwa 40 au  zaidi ambapo imeweza  kuongoza kiwilaya kuwa ya kwanza na kimkoa ya 6.
Mkurugenzi  huyo alisema  kuwa ajili ya kuwashukuru  wazazi  wanaosomesha   watoto  wao katika shule  hiyo wameamua  kutoa punguzo ya ada kwa  wanafunzi hao  waliofaulu mtihani wa darasa la  saba ambao  watajiunga na shule ya  Sekondari ya Southern Highlands Mafinga  ,huku  akiwaomba   wazazi  wenye  watoto  wanaohitaji  kujiunga na shule   hiyo kuwapeleka  watoto  wao kwani shabaha kuu ni  kuona  watoto  wanaendelea  kupata  elimu bora.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.