MBUNGE WA CHALINZE, RIDHIWANI KIKWETE AKABIDHI MAGODORO 200 KWA SHULE YA MORETA


Mbunge wa jimbo la Chalinze Ridhiwani  Kikwete akikabidhi  magodoro kwa wanafunzi na mwalimu Mkuu wa shule ya sekondari Moreto ,Justine Lyamamu ,ambapo  bweni la  wasichana katika shule hiyo liliungua wiki iliyopita.

Mbunge wa Chalinze Ridhiwani akifurahia jambo na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya chalinze, Mkurugenzi na maafisa wengine wa halmashauri ya Wilaya Chalinze.
Mbunge wa chalinze ametimiza ahadi yake ya kuchangia magodoro 200 na Halmashauri ya wilaya ya chalinze kwa shule ya Sekondari ya Moreto.
Mbunge akisema neno la ushauri na kuwatia moyo vijana kwa tukio lililowakuta na kwa utulivu uliotokea.
Wanafunzi wa shule ya sekondari Moreto  iliyopo Lugoba wilayani Bagamoyo, Mwanahamis Msonde na Sekion Mponela wakimshukuru Mbunge wa jimbo la  Chalinze Ridhiwani  Kikwete na mwenyekiti wa halmashauri ya Chalinze Saidi  Zikatimu kwa msaada wa magodoro.

Na Mwamvua Mwinyi.


MBUNGE wa jimbo la Chalinze ,Ridhiwani Kikwete kwa kushirikiana na halmashauri ya Chalinze,wametoa magodoro 200  yaliyogharimu zaidi ya mil.8 ili kuwasaidia wanafunzi wa shule ya sekondari ya Moreto iliyopo Lugoba wilayani Bagamoyo.

Aidha Ridhiwani ameahidi kushirikiana na wadau pamoja na halmashauri hiyo,kujenga bweni jipya la wanafunzi wa kike,shuleni hapo baada ya kuunguliwa na bweni wiki iliyopita.
Sambamba na hayo tathmini imebaini hasara ya sh.mil 74 baada ya bweni hilo kuungua  na kusababisha mali zote kuteketea kwa moto.

Akikabidhi magodoro hayo ,kwa mwalimu mkuu wa shule hiyo,Justine Lyamuya ,mbunge huyo alisema kati ya magodoro hayo 136 yatatumiwa na wanafunzi wa kike na yatakayobaki yatatumika na wanafunzi wa kiume.

Ridhiwani alisema mara baada ya kutokea kwa janga hilo, alitoa magodoro 50 yenye thamani ya mil.2.2 kwa nguvu zake mwenyewe.

Hata hivyo aliwataka wanafunzi hao kushirikiana na serikali na vyombo vya dola kuwafichua waliohusika na tukio la kuchoma moto bweni.

Ridhiwani alielezea kuwa serikali itahakikisha waliohusika kuchoma moto bweni hilo,wanatafutwa ili wakamatwe na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.

Alisema tukio hilo linasikitisha na kurudisha nyuma juhudi za serikali na wadau mbalimbali wa elimu wanaohakikisha  wanafunzi wanakaa bweni .

“Tumeweka mikakati ya kuhakikisha tunawakamata wale wote waliohusika na tukio hili baya na matukio haya ni mwendelezo wa uunguzaji wa shule ambapo Chalinze imechomwa mara mbili,” alisema Ridhiwani.

Ridhiwani aliwaomba wadau mbalimbali kujitokeza kushirikiana kutatua changamoto zilizojitokeza shuleni humo.

Nae  mwalimu mkuu wa shule hiyo Justine Lyamuya alifafanua kuwa vitu vyote viliungua ikiwa ni pamoja na vitanda na magodoro 75 vyenye thamani ya mil. 24.

Alisema bweni hilo lilijengwa hivi karibuni kwa thamani ya mil.50 ambalo limeungua lote na halifai tena kutumika.

“Moto huo uliunguza vitu vyote vilivyokuwemo ikiwepo magodoro, vitanda 75, madaftari, vitabu, nguo na vifaa vingine lakini mungu alisaidia kati ya wanafunzi 196 wanaolala bweni hili,hawakuwepo bwenini,” alisema Lyamuya.

Mwenyekiti wa halmashauri ya Chalinze,Said Zikatimu alisema licha ya kuchangia magodoro hayo tayari wameitisha kikao na wazazi, walezi na wadau wa elimu ili kujadili namna ya kukabiliana na tatizo hilo.

Baadhi ya wanafunzi Sekion Mponela na Mwanahamis Msonde walimshukuru mbunge wa Chalinze na halmashauri kwa msaada walioutoa na kuahidi kutunza magodoro hayo.

Octoba 5 mwaka huu majira ya asubuhi moto ulizuka katika bweni la wanafunzi wa kike shuleni humo na kusababisha hasara kubwa.
Mwisho.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.