MFALME MOHAMMED VI WA MOROCCO AAHIDI KUJENGA UWANJA WA KISASA DODOMA


Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
MFALME Mohammed VI wa Morocco amekubali kujenga Uwanja wa kisasa wa mpira wa miguu katika makao makuu ya nchi mjini Dodoma.
Hayo yamesemwa leo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Joseph Magufuli katika hafla fupi ya kusaini makubaliano mbalimbali ya kibiashara kati ya Tanzania na Morocco iliyofanyika Ikulu mjini Dar es salaam.
Akizungumza mbele ya Mfalme huyo ambaye alikuja nchini jana jioni, Rais Magufuli alisema kwamba alimuomba msaada wa kujenga Uwanja wa kisasa wa mpira wa miguu mjini Dodoma, ombi ambalo limekubaliwa.

Ujenzi wa Uwanja huo wa kisasa utagharimu kati ya sh. Bilioni 174 na 228.
Rais Magufuli (kulia) akiwa na mgeni wake, Mfalme Mohamed V wa Morocco Ikulu mjini Dar es salaam

Mfalme huyo aliwasili nchini nchini Oktoba 23, 2016 kwa ziara ya kiserikali ya siku tatu kwa mwaliko wa Rais Magufuli.
Alitua Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere mjini Dar es Salaam majira ya saa 11 Jioni na kupokewa na mwenyeji wake, Rais Magufuli kabla ya kupigiwa mizinga 21 na kukagua gwaride rasmi la Jeshi la Wananchi Tanzania lililoandaliwa kwa heshima yake.
Leo jioni Mfalme Mohammed VI atashiriki dhifa ya kitaifa aliyoandaliwa na Mwenyeji wake Rais Magufuli.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.