Taassisi ya MOI imefanikiwa kufanya upasuaji wakunyoosha mfupa wa mgongo wa mtoto hivi karibuni uliopinda (Kibiongo) kitaalamu (Scoliosis). kupitia madaktari bingwa wa MOI walioko kwenye mafunzo ya ubobezi wa juu katika upasuaji wa mifupa na mgongo kwa watoto kwa kushirikiana na madaktari bingwa kutoka Marekani(PICHA NA MAKTABA MOI)
10/12/2016,
Dar es Salaam, Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) kwa mara ya kwanza
imefanya upasuaji mkubwa kwa mafanikio makubwa wa kunyoosha mfupa wa mgongo wa
mtoto uliopinda (Kibiongo) kitaalamu (Scoliosis).
Upasuaji
huo umefanyika kwa kutumia technolojia ijulikanayo kama ‘Posterior
Instrumentation and Fusion’ ambayo inahusisha uwekaji wa vyuma maalum kwenye
mfupa wa mgongo uliopinda katika sehemu ya juu na chini ya mfupa wa mgongo na kuufanya mgongo unyooke kama inavyotakiwa
Taassisi
ya MOI imefanikiwa kufanya upasuaji huo kupitia madaktari bingwa wa MOI walioko kwenye
mafunzo ya ubobezi wa juu katika upasuaji wa mifupa na mgongo kwa watoto kwa kushirikiana na madaktari bingwa kutoka
Marekani
Aidha,
Uanzishwaji wa upasuaji huu umetokana na kuanzishwa kwa ushirikiano wa
kimafunzo kati ya Taasisi ya MOI na Chuo cha madaktari bingwa wa upasuaji cha
Afrika Mashariki , Kati na Kusini ‘COSECSA’ na Madaktari bingwa kutoka Marekani
Uanzishwaji
wa upasuaji huu wa kunyoosha migongo ya watoto iliyopinda (Scoliosis) unatarajiwa
kuisaidia serikali kupunguza rufaa za kuwapeleka wagonjwa nje ya nchi ambazo ni
za gharama kubwa. Ambapo gharama za kumtibu mtoto mmoja nje ya nchi ni zaidi ya
dola za kimarekani elfu 30 hadi 40
Hivyo,
Uongozi wa Taasisi ya MOI unatoa wito kwa madaktari kwote nchini kuja kupata
mafunzo hayo hapa MOI, Pia wazazi wenye watoto wenye matatizo hayo wawalete
hospitali ili wafanyiwe uchunguzi na upasuaji
-xxxx-
Imetolewa
na,
Patrick
J. Mvungi
Comments