MSEMAJI WA SERIKALI: WAZIRI HATOKUWA NA MAMLAKA MAKUBWA KATIKA MUSWADA WA HABARI



Mkurugenzi wa Habari, Hassan Abbas (mwenye suti) akizungumza katika ya kipindi mahojiano maalum cha 360 kinachorushwa na kituo cha Televisheni cha CLOUD wakati wa ziara yake ya kutembelea vyombo vya habari Jijini Dar es Salaam na kuelezea maudhui mbalimbali yaliyopo katikamuswada ya sheria ya huduma ya Habari. Wengine ni Watangazaji wa Kituo hicho, Babbie Kabae (kushoto) na Hassan Ngoma. 
Mkurugenzi wa Habari, Hassan Abbas akibadilishana mawazo na Watangazaji wa kipindi cha Michezo cha kituo cha Redio cha CLOUDS FM cha Jijini Dar Es Salaam, kutoka kutosho Shafii Dauda (kulia) na Mbwiga mbwiguko (katikati) wakati wa ziara yake ya kutembelea vyombo mbalimbali vya habari leo Jijini Dar es Salaam. Katika ziara hiyo Msemaji huyo wa Serikali alizungumzia maudhui mbalimbali yaliyopo katika muswada wa sheria ya huduma ya habari. 
Mkurugenzi wa Habari, Hassan Abbas (mwenye suti) akiwa katika picha ya pamoja na Wahariri na Waandishi wa Habari wa kituo cha habari cha Redio na Televisheni cha CLOUD wakati wa ziara yake ya kutembelea vyombo vya habari leo Jijini Dar es Salaam. Katika ziara hiyo Msemaji huyo wa Serikali alizungumzia maudhui mbalimbali yaliyopo katika muswada wa sheria ya huduma ya habari. 
Mkurugenzi wa Habari, Hassan Abbas akipokelewa na Meneja vipindi wa kituo cha redio cha Times FM cha Jijini Dar es Salaam, Amani Misana wakati wa ziara yake ya kutembelea vyombo mbalimbali vya habari leo Jijini Dar es Salaam. Katika ziara hiyo Msemaji huyo wa Serikali alizungumzia maudhui mbalimbali yaliyopo katika muswada wa sheria ya huduma ya habari. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Redio cha Times FM cha Jijini Dar es Salaam, Rehure Nyaulawa akifafanua jambo kwa Mkurugenzi wa Habari, Hassan Abbas kuhusu utendaji kazi wa gari la urushaji matangazo ya nje. Katika ziara hiyo Msemaji huyo wa Serikali alizungumzia maudhui mbalimbali yaliyopo katika muswada wa sheria ya huduma ya habari.

Mkurugenzi wa Habari, Hassan Abbas akizungumza katika ya kipindi mahojiano maalum ya kipindi cha Hatua Tatu kinachorushwa na kituo cha Redio cha Times FM cha Jjijini Dar es Salaam kuelezea maudhui mbalimbali yaliyopo katikamuswada ya sheria ya huduma ya Habari. Anayefuatilia mahojiano hayo ni mahojiano hayo ni mtangazaji wa kituo hicho Stanslaus Lambat. 
Mkurugenzi wa Habari, Hassan Abbas akiwa katika picha ya pamoja na Bodi ya Uhariri ya Kituo cha Redio cha Times FM cha Jijini Dar es Salaam wakati wa ziara yake ya kutembelea vyombo mbalimbali vya habari Jijini Dar es Salaam. Katika ziara hiyo Msemaji huyo wa Serikali alizungumzia maudhui mbalimbali yaliyopo katika muswada wa sheria ya huduma ya habari.

(PICHA NA ISMAIL NGAYONGA)

………………………………………………………………………………

Na Beatrice Lyimo-MAELEZO-Dar es Salaam

SERIKALI imesema hakutokuwa na matumizi mabaya ya mamlaka anayopewa Waziri anayesimamia tasnia ya habari katika muswada wa sheria ya huduma ya habari isipokuwa kwa masuala yatakayohatarisha usalama wa Taifa.

Imesema Serikali haiwazuii waandishi wa habari kukosoa sera, matamko na ahadi mbalimbali zinazotolewa na Viongozi wa kitaifa pindi wanaposhindwa kutekeleza maagizo wanayoyatoa kwa wananchi.

Akizungumza katika mwendelezo wa ziara yake ya kutembelea vyombo mbalimbali vya habari leo Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Hassan Abbas alisema muswada huo unatoa fursa kwa chombo cha habari kupeleka malalamiko yake mahakamani pindi inapotokea kutokubaliana na hatua itakayoweza kuchuliwa na Waziri mwenye dhamana ya habari.

Kwa mujibu wa Abbasi alisema yapo masuala kadhaa yanayopaswa kuchuliwa hatua za haraka za maamuzi ikiwemo suala la uchochezi, uasi wa kikundi fulani cha watu kinachotaka kuigombanisha Serikali na wananchi.

Aliongeza kuwa hata katika mikataba ya kimataifa ikiwemo kifungu cha 19 mkataba wa geneva wa mwaka 1966 umeeleza kuhusu haki ya kupata habari na taarifa ingawa upo ukomo katika masuala kadhaa ikiwemo suala la usalama wa taifa.

“Uchochezi ni kuhatarisha amani ya nchi, lakini mwandishi akiikosoa Serikali haitokuwa uchochezi bali kwa atakayeleta habari za uchochezi kwa maana ya uasi atatakiwa kuwajibishwa” alifafanua Mkurugenzi Abbas.

Aidha alisema kuwa muswada huo umekusudia kuanzishwa kwa Baraza la Maadili litakalokuwa na wajumbe saba, ambapo wanne kati yao ni kutoka katika tasnia ya habari ikiwemo mwenyekiti wa Baraza na watakuwa na mamlaka ya kusimamia maslahi na usalama wa waandishi.

Akifafanua zaidi alisema kuwa lengo la Serikali ni kuhakikisha kuwa mchakato wa kupata Sheria ya huduma ya habari unafika mwisho ambapo mchakato wake umechukua miaka 20 mpaka sasa.

Alisema kuwa lengo la Serikali ni kuhakikisha kuwa muswada huo unapitishwa na Bunge ili uweze kuwa sheria kamili na hatimaye kuifanya tansia ya habari kuwa taaluma yenye kuheshimika zaidi.

Pia alisema kuwa muswada huo utasaidia sekta ya habari kuwa muhimili wenye nguvu na taaluma iliyokamilika yenye haki zake kama upatikaji wa bima za afya kwa waandishi wa habari.

Abbasi alisema iwapo sheria hiyo itapitishwa itatumika upande wa Tanzania Bara pekee na si Zanzibar, kwa kuwa suala la habari halipo katika mambo ya Muungano, ingawa sekta hizo zinashirikiana kwa namna moja au nyingine

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI