MSIKIMBILIE KWA WAGANGA WA KIENYEJI MKIUMWA-DC RUFIJI


Rais wa taasisi inayojishughulisha kutoa huduma za tiba za macho,presha ,kisukari na huduma za kijamii ,Lions club Dar es salaam -Pwani ,Lion Reshma Shah ,akizungumza jambo katika kambi  ya kutoa  huduma za tiba  ya magonjwa hayo bila malipo huko Ikwiriri Rufiji Mkoani Pwani. (Picha na Mwamvua Mwinyi)

Na Mwamvua Mwinyi,Rufiji
MKUU wa wilaya ya Rufiji,Juma Abdallah ametoa rai kwa wananchi wilayani humo,kuacha tabia ya kukimbilia kwa waganga wa kienyeji mara wanapoumwa magonjwa mbalimbali  na badala yake wawahi kwenye vituo vya afya kwa ajili ya uchunguzi na utalaamu zaidi.
Aidha amesema muda wa uchaguzi umepita hivyo amewataka viongozi wa kuchaguliwa ikiwemo wabunge na madiwani kuacha tabia ya kuendekeza siasa bali wafanye kazi kuleta maendeleo.
Abdallah alisema hayo ,wakati taasisi ya Lions club inayojishugulisha kutoa tiba ya magonjwa ya macho,presha na kisukari walipoweka kambi ya kutoa tiba bure ya magonjwa hayo Ikwiriri wilayani Rufiji.

Alisema hakuna sababu ya kuamini kuwa ukiugua magonjwa hayo basi kuna mambo ya kimila hali inayosababisha matatizo ya kiafya kukua na wakati mwingine kupelekea kifo.
Abdallah alieleza kuwa magonjwa ya macho ,presha na kisukari yanatibika kitaalamu na sio kwa njia za kienyeji.
“Kwa waganga wa kienyeji hakuna microscope, huko hakuna vifaa vya kutibu matatizo hayo,ukija kuchoka unakuta umeshaharibikiwa na ugonjwa unakuwa tayari umekua”

“Ni rai yangu kwenu mkimbilie kwenye vituo vya afya,na pia muache uchafu kwani inzi,chawa,kunguni,wanapenda kukaa kwenye uchafu na uchafu unachangia kupata magonjwa yanayotokana na uchafu”alisema mkuu huyo wa wilaya.
Abdallah aliwaasa wananchi hao kujiimarisha kwenye usafi wa mazingira na kuhakikisha wanafanya usafi wa ndani ya nyumba zao,miili na mazingira yanayowazunguka.
Mkuu huyo wa wilaya aliisihi jamii pia kujitokeza kujiunga na mfuko wa CHF kwa gharama ya sh.10,000 ili kupata huduma za kiafya kirahisi ndani ya wilaya.
Abdallah alieleza wilaya hiyo ipo nyuma kwa asilimia 13 kwa watu waliojitokeza kuchangia kwenye mfuko huo ,wakati matakwa ya kiuongozo inataka asilimia 30 kila wilaya.
Hata hivyo aliitaka Lions club kupanua wigo wa kutoa huduma katika wilaya ya Rufiji na mikoani kwani wapo watu wengi wasio na uwezo wenye mahitaji ya huduma za kiafya bure.
Rais wa Lions club ,Lion Reshma Shah,aliwashukuru watu kujitokeza katika kambi hiyo na lengo lao ilikuwa kutibia watu 600 ambapo wamefikia lengo lengo lao.
Alisema walishatoa huduma zao jijini Dara es salaam na Rufiji Pwani na wana jumla ya club 48 wakisaidia tiba ya macho,kisukari,presha na kutoa huduma mbalimbali za kijamii ikiwemo kutoa misaada ya miwani,chakula,maji.
Lion Reshma alisema kutoa sio ufahari lakini wanajitolea kutokana kwamba wanafahamu kwa kutoa tiba hizo inawasaidia wale wasio na uwezo.
Mganga mkuu wa wilaya hiyo,dk.Julius Sewangi,alisema tatizo la macho ni kubwa ambalo linasababisha upofu,uoni hafifu,ulemavu na kusababisha vifo .
“Ugonjwa wa macho ni miongoni mwa tatizo kubwa wilayani ambapo mtoto wa jicho kwa mwaka 2015 walikuwa na wagonjwa 22 na hadi sept 2016 kulikuwa na wagonjwa 24 ikiwa ni ongezeko la wagonjwa wawili”alieleza.

Dk.Sewangi alisema mwaka 2015/2016 kulikuwa na wagonjwa wa macho 700 kati ya idadi hiyo wazee ni asilimia 78.3 na watoto ni asilimia 21.7.
Aliwashukuru wadau wanaoshirikiana kuwaongezea nguvu kwa kuendesha kambi za uchunguzi na matibabu sanjali na Lions,CCBRT na Bilal muslim.
Alisema ushirikiano huo umewezesha kupunguza magonjwa ya macho ambayo yanaambukiza na kutibu magonjwa ya kisukari,presha na macho na kutoa elimu.
Dk.Sewangi alifafanua magonjwa yasioambukiza hali sio nzuri kutokana na mfumo wa maisha ambao watu wanaishi kwa kula vyakula zaidi ya mahitaji ya mwili,vyenye mafuta,chumvi ,kuvuta tumbaku,kunywa pombe kupita kiasi na kutofanya mazoezi.
Alisema kutokana na changamoto hizo idara ya afya imekuwa na mikakati ya utoaji elimu endelevu kwenye vituo vinavyotoa huduma za afya,kuimarisha huduma na kliniki za magonjwa hayo .

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA