MTANGAZAJI WA BBC AWA MENEJA MKUU AZAM FC


Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
MTANGAZAJI wa zamani wa Idhaa ya Kiswahili ya Shirika la Utangazaji Uingereza (BBC), Abdul Mohammed leo ametambulisha kuwa Meneja mpya wa klabu ya Azam FC ya Dar es Salaam.
Uteuzi huo ulioanza Oktoba 1, mwaka huu ni sehemu ya mikakati ya Azam FC ya kujiendesha kiueledi na wakiamini ujio wa Mohamed atayeingia kwenye sekretarieti ya timu, utaongeza nguvu kwenye eneo la uongozi na hatimaye kufikia malengo tuliyoyakusudia.
Azam FC inaamini katika uendeshaji mambo kiueledi ndani ya klabu na ndio maana imekuwa na safu ya uongozi iliyosheheni watu wenye taaluma mbalimbali.
Abdul Mohammed (kulia) akiwa na Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Saad Kawemba

Hivyo tunaamini kwa uzoefu aliokuwa nao Mohamed huko alikotoka akiwa kama mwandishi wa habari kwenye Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) na nguvu kazi ya viongozi wengine utaweza kutufikisha kwenye mafanikio.
Majukumu ya kuendesha klabu kila siku yamekuwa na changamoto mpya zinazohitaji kutatuliwa kupitia nguvu kazi ya watu na Azam FC haitasita kuboresha mfumo wake wa uendeshaji wa klabu ili kuendana na changamoto hizo, kwa kuuongezea nguvu kazi pale inapohitajika ili kufikia mafanikio.
Mbali na kufanya kazi kwa muda mrefu kwenye sekta ya habari akipita IPP Media, Clouds Media na BBC, Mohamed pia amesomea masuala ya Uhasibu na Fedha. Azam FC inamtakia kila la kheri kwenye majukumu yake mapya hayo katika ngazi ya soka.
0

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MATOKEO YA KIDATO CHA PILI, DARASA LA SABA YATANGAZWA ZANZIBAR

HIVI NDIVYO BIASHARA YA NGONO NAMNA INAVYOTIKISA MOROGORO: SEHEMU YA PILI.

ZAIDI YA WANANCHI 500 KUSHIRIKI MAFUNZO YA MKIKITA YA KILIMO CHA PAPAI SALAMA

MKIKITA YATOA OFA KWA KILA HEKA YA PAPAI SH. MIL. 2 KUTANDAZA MIUNDOMBINU YA UMWAGILIAJI

DIAMOND AITWA NA NYOTA YAJAA GOMS

WATEJA WA NSSF DAR WATIMULIWA KWA MTUTU WA BUNDUKI

MATOKEO YA DARASA LA SABA YATANGAZWA

KAMISHNA MARIJANI AZINDUA CHAMA CHA WAFUGAJI MBWA TANZANIA (TCA)