MTOTO AMWAGIWA PETROLI KISHA KUWASHWA NA MWAJIRI WAKE


Image result for KAMANDA WA POLISI MKOA WA ARUSHA
Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Charles Mkumbo

Na  Woinde  Shizza,Monduli
Jeshi la mkoani Arusha linawashikilia watu Wa nne akiwemo mmiliki Wa Kambi ya LILAC inajishulisha na maswala ya utalii mto Wa mbu John Kadozo(46) mwenye asili ya kiasia mkazi Wa mto Wa mbu wilayani Monduli kwa kosa la kumchoma kwa kumwagia petroli mfanyakazi wake.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda Wa Polisi mkoa Wa Arusha Charles Mkumbo alisema kuwa tukio hilo lilitokea October 9 majira ya saa nne Usiku ndani ya Kambi ya mtuhumiwa iliopo mto Wa mbu wilayani Monduli.
alisema kuwa mtumiwa alimchoma moto mtoto aliyejulika kwa jina la Paskali Alfonce (17) mkazi Wa mto Wa mbu  aliyekuwa mpishi Wa kampuni yake kwa kosa la kuchelewa kubandika maharage.
"Inasemakana kijana huyu alikuwa mpishi Wa pale sasa Siku hiyo alipewa fedha akanunue maharage alipoenda alichelewa kurudi ndipo mtuhumiwa na wenzake walipomkamata kijana Huyo na kumwagia petroli kisha kumuwasha "alisema mkumbo
Aliwataja watuhumiwa wengine ambao walishirikiana kufanya tukio hilo na wote wanashikiliwa na jeshi la polisi kuwa ni John Kadozo (46),George Kessy (28) Martin Petro (16) Enock Wilium (19) na watuhumiwa wote wapo mahabusu na wanatarajiwa kufikishwa mahakamani mapema iwezekanavyo .
Akisimulia tukio niko kwa uchungu mtoto Alfonce ambaye amelazwa katika hospitali Seliani  iliopo ngaramtoni alisema siku hiyo alitumwa maharage ila alichelewa kurudi kutokana na kuyakosa lakini aliporudi ndipo walipomkamata na kumfunga shuka mikono wakamwagia petroli kisha kumchoma
"Nilibahatika kuchoropoka nikakimbia sasa Jirani na hapo kuna mfereji nika rukia uko ndio nikazimika maana niliwaka kabisa "alisema mtoto Alfonce
huku akilia kwa uchungu. 
Mama mlezi aliyejitambulisha kwa jina la Cristina Faustine alisema anasikitika sana maana amemlea huyo mtoto kwa shida tangu wazazi wake wafariki na aliamua amruhusu kwenda kufanya kazi ili aweze kujikimu na aweze kujipatia maitaji yake.
Aidha alitumia mud a huo kuiomba serekali kuakikisha mtoto uyo anapata matibabu na kwani kwasasa anauwezo wakugaramia matibabu ya uyo mtoto.
0

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MATOKEO YA KIDATO CHA PILI, DARASA LA SABA YATANGAZWA ZANZIBAR

HIVI NDIVYO BIASHARA YA NGONO NAMNA INAVYOTIKISA MOROGORO: SEHEMU YA PILI.

ZAIDI YA WANANCHI 500 KUSHIRIKI MAFUNZO YA MKIKITA YA KILIMO CHA PAPAI SALAMA

MKIKITA YATOA OFA KWA KILA HEKA YA PAPAI SH. MIL. 2 KUTANDAZA MIUNDOMBINU YA UMWAGILIAJI

WATEJA WA NSSF DAR WATIMULIWA KWA MTUTU WA BUNDUKI

PICHA:NYOKA AINA YA CHATU AUWAWA KANISANI BAADA YA KUKUTWA NYUMBANI KWA MFANYABIASHARA MAARUFU JIJINI ARUSHA AKISADIKIWA KWA IMANI ZA KISHIRIKINA

KAMISHNA MARIJANI AZINDUA CHAMA CHA WAFUGAJI MBWA TANZANIA (TCA)

MATOKEO YA DARASA LA SABA YATANGAZWA