TANZANIA NA UGANDA WASAINI MKATABA WA UTEKELEZAJI UJENZI WA BOMBA LA MAFUTA

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (wa Tatu kushoto mstari wa Mbele) na Waziri wa Nishati na Maendeleo ya Madini wa Uganda, Mhandisi Irene Muloni (wa Pili kushoto mstari wa mbele) wakitoka katika eneo la Chongoleani mkoani Tanga baada ya kukagua sehemu itakayojengwa hifadhi ya mafuta pamoja na gati itakayotumika kupakia mafuta kwenye Meli mbalimbali baada ya kusafirishwa na Bomba la Mafuta kutoka nchini Uganda.


Serikali ya Tanzania na Uganda  kwa pamoja wamesaini mkataba wa makubaliano ya namna ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa  bomba la mafuta ghafi unaotarajiwa  kuanza hivi karibuni  kutoka Ziwa Albat mpaka bandari ya Tanga.
Mkataba huo umesainiwa mara baada ya kumalizika kwa kikao kilichodumu kwa siku tatu kati serikali ya Tanzania na Uganda kilichofanyika mkoani humo katika ukumbi wa hotel ya Tanga beach resort.
Makataba huo umesainiwa na waziri wa nishati na madini Profesa Sospeter Muhongo pamoja na waziri wa nishati na madini nchini Uganda Irene Muloni.
Akizungumza mara baada ya kusaini mkataba huo Waziri wa nishati na madini nchini Tanzania Sospeter Muhongo alisema mkataba huo umegusa maeneo mbali mbali muhimu ikiwemo upatikanaji wa ardhi ,ulinzi pamoja na uwekezaji.
profesa Muhongo alisema Serikali ya  pande zote mbili  inashirikiana kwa ukaribu katika kuhakikiasha mradi huo unakamilika kwa wakati na kuanza kufanya kazi ifikapo mwaka 2020.
"Mradi upo na kasi ya utekelezaji inatendeka lengo ni kuhakikisha ifikapo mwaka 2020 mradi umekamilika na hivyo basi kwa sasa ni wakati wa kila mtu kuwa tayari kwaajili ya mradi huu"alisema Muhongo
Kwa upande wake Waziri wa nishati na madini nchini Uganda Irene Muloni alisema amefurahi kuona namna ambavyo wananchi wa  nchi zote mbili walivyokuwa na shauku ya kuupokea mradi huo.
"Jana nimetembelea maeneo mbalimbali ya jiji la Tanga ikiwemo bandari pamoja sehemu ambayo bomba la mafuta litapita na nimeona ni jinsi gani wananchi wameufurahia mradi huu hivyo ni wakati sasa wa kufanya kazi na wananchi wa Tanzania na Uganda wajiandae"alisema Muloni
Mwisho.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI