Uchaguzi wa Marekani 2016: Yote unayofaa kujuaUchaguzi mkuu nchini Marekani
Image captionUchaguzi mkuu nchini Marekani
Mnamo mwezi Januari 2017 ,taifa lenye nguvu zaidi duniani litakuwa na kiongozi mpya baada ya uchaguzi wenye ushindani mkali na gharama kubwa-lakini Uchaguzi wa Marekani hufanyika vipi?
Wakati Marekani inapomchagua kiongozi wake ,haichagui kiongozi wa taifa pekee bali kiongozi wa serikali pamoja na kamanda wa jeshi kubwa zaidi duniani.Ni wajibu mkubwa sana.
 • Kwa hivyo hatua hiyo hufanyika vipi?
 • Nani anaweza kuwa rais?
Kwa mtu kufaulu kuwania urais ,unahitaji kuwa mzaliwa mwenye asili ya Marekani,uwe na umri wa kuanzia miaka 35 na uwe mkazi wa taifa hilo kwa takriban miaka 14.Inaonekana kuwa rahisi sana sio?
Ukweli hatahivyo ni kwamba, takriban kila rais tangu mwaka 1933 amewahi kuwa gavana ,seneta ama hata jenerali wa jeshi.
Hilo ni kabla ya kufikiria kupata uteuzi mbali na kuvutia vyombo vya habari.
Katika uchaguzi wa mwaka 2016,katika hatua moja kulikuwa na magavana 10,ama waliokuwa magavana na maseneta 10 ama maseneta wa zamani,ijapokuwa wengi waliondolewa na wengine hata kujiuzulu.
Mtu mmoja huteuliwa kuwakilisha chama cha Republican ama hata Democrat katika uchaguzi wa urais.
 • Jinsi ya kuwa rais wa Marekani.
 • Ni Nani anayeteuliwa kuwakilisha kila chama.
Msururu wa chaguzi hufanywa katika kila jimbo pamoja na maeneo ya nga'mbo,kuanzia mwezi Februari ambao huamua ni nani anayewakilisha kila chama kama mgombea wa urais.
Mshindi kila chama hupata wajumbe kadhaa walio na uwezo kumpigia kura mgombea huyo katika mkutano mkuu wa chama hicho unaofanyika mwezi Julai,ambapo wagombea hao huidhinishwa rasmi.
Ni wakati huohuo ambapo makamu wa rais pia huteuliwa ambapo Bi Clinton alimchagua seneta Tim Kaine wa Virginia,naye Trump akimteua gavana Mike Pence wa Indiana kwa upande wa Republican.
 • Maswala muhimu katika kampeni.
Kumekuwa na maswala tata yaliozushwa na mgombea wa Republican Donald Trump tangu mfanyiabishara huyo wa New York kuzindua kampeni yake yenye maelezo kwamba wahamiaji kutoka Mexico ni ''wabakaji na wahalifu''.
Mgombea huyo hajawahi kumaliza wiki moja bila kuzua hisia kali.
Amewahi kurushiana maneno na jaji mmoja,Malkia wa urembo ,mtangazaji wa runinga ya Fox pamoja na familia ya mwanajeshi mmoja aliyefariki nchini Iraq.
Pia amelazimika kutetea hatua yake ya kutoweka wazi kodi ambayo amekuwa akilipa kwa kipindi cha miaka 18,pamoja na maswali yanayozunguka mashirika yake ya hisani.
Hillary Clinton naye amekumbwa na nyakati za kutia wasiwasi.
Uharibifu uliosababishwa na barua pepe zake za kibinfasi ni mkubwa mno ,na maswali yameulizwa kuhusu mchango kutoka mataifa ya kigeni unaoingia katika hazina ya Clinton.
Gazeti la New York Times ambalo linamuunga mkono limekuwa likiangazia hatua alizochukua kumnyamazisha mwanamke ambaye alidai kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mumewe Bill.
 • Ni nani aliyeshinda mdahalo wa kwanza?
Mdahalo wa kwanza uliofanyika mjini New York mnamo mwezi Septemba uliwaleta pamoja wagombea hao wawili kwa mara ya kwanza na watazamaji walifurahi.
Trump na Clinton walikabiliana kwa dakika 97,huku mgombea huyo wa Demokrat akionekana kumuingilia sana Trump,kupitia kumshutumu kwa kuwanyanyasa wajenzi ,kupitia kuficha kodi anayofaa kulipa na kuwa mbaguzi dhidi ya wanawake.
Hatahivyo Trump kutoka New York alimkabili vikali Clinton kuhsu mipango yake ya biashara,barua pepe na kuhusu eneo la Mashariki ya kati, akimtaja kuwa mwanasiasa ambaye hana ufanisi wowote baada ya miongo mitatu ya maisha yake ya uma.
Wachanganuzi waliokuwa wakiangalia na kung'amua ni nani anayesema ukweli,pamoja na BBC walifanya kazi yao ya ziada kuhusu madai muhimu.
Hillary Clinton anaongoza katika kura ya maoni kwa asilimia 49 dhidi ya Trump mwenye asilimia 44Image copyrightEPA
Image captionHillary Clinton anaongoza katika kura ya maoni kwa asilimia 49 dhidi ya Trump mwenye asilimia 44
 • Ni tarehe gani muhimu kati ya sasa na tarehe ya uchaguzi huo?
Inaonekana kana kwamba tumepitia kipindi kirefu cha kampeni za uchaguzi,Lakini ukweli ni kwamba ndio mwanzo tu mkono unaalika maua-pole.
Kutakuwa na midahalo mitano zaidi itakayopeperushwa katika runinga katika wiki tano za mwisho:
 • Tarehe 4 mwezi Oktoba utafanyika huko Farmville,Virginia{Mdahalo wa makamu wa rais}
 • Tarehe 9 mwezi Oktoba huko St Louis Missouri
 • Tarehe 19 Oktoba mjini Las Vegas,Nevada
 • Na hatimaye-Kura zitaanza kupigwa tarehe 8 Novemba.
Mgombea mwenye kura nyingi katika kila jimbo ndio mgombea wa urais anayeungwa mkono na jimbo hilo.
Kazi yote itawachiwa kundi la watu 538 {Electoral College} watakaomchagua rais.
Nusu yao ambayo ni 270 inahitajika kwa rais kuchaguliwa.
Lakini sio majimbo yote yako sawa, kwa mfano jimbo la Carlifonia,lina zaidi ya mara 10 ya idadi ya watu katika jimbo la Connecticut,kwa hivyo hawapati fursa sawa ya usemi.
Kila jimbo lina idadi kadhaa ya wapigaji kura hao {electors},ambao hutokana na idadi ya watu wa sehemu wanazotoka.
Wakati raia wanapomchagua mgombea wao ,huwa wanawapigia kura wajumbe hao.
 • Lakini hapa ndio pale ambapo huwavutia watu.
Karibia kila Jimbo isipokuwa Nebraska na Maine,mshindi hushinda kila kitu,kwa hivyo mtu anayeshinda wajumbe wengi au electors mjini New York ,kwa mfano atapata kura zote za wajumbe 29.
Katika kinyang'anyiro cha kushinda wajumbe {electors} 270, ni majimbo yasio na mgombea wa moja kwa moja anayeungwa mkono ambayo huamua ni nani mshindi.
 • Ni Majimbo gani hayo?
Tuna,wagombea wawili wote wakipigania wajumbe 270 kwa kushinda kila jimbo.Vyama vyote vinafikiri vinaweza kutegemea majimbo kadhaa,yawe makubwa ama hata madogo.
Republican inategemea kushinda katika jimbo la Texas, na chama hicho hakitumii muda wao mwingi na fedha kujaribu kufanya kampeni katika eneo hilo.
Vilevile Jimbo la Carlifornia hutegemewa sana na wagombea wa Demokrat.
Raia wa Marekani wakifuatilia kampeni za wagombea wao moja kwa moja
Image captionRaia wa Marekani wakifuatilia kampeni za wagombea wao moja kwa moja
Majimbo mengine huitwa ''Swing States''ambapo mgombea yeyote anaweza kushinda.
Kwa mfano jimbo la Florida lenye wajumbe 29,lina umaarufu kwa kuamua uchaguzi wa 2000 ambapo George W.Bush aliibuka mshindi,baada ya kupoteza kura ya kitaifa ,kabla ya mahakama ya juu kuonyesha kuwa alikuwa ameshinda kura ya wajumbe au 'electoral votes'.
 • Ni lini rais mpya huanza kufanya kazi?
Katika siku na wiki baada ya uchaguzi,iwapo kura hiyo inatoa mshindi wa moja kwa moja,mshindi huyo atabuni baraza la mawaziri na kuanza kuandika sera zenye ajenda yake.
Wakati huohuo rais anayeondoka anafanya kazi ya kuinoa sifa yake na kuanza kuondoka katika afisa ya rais.
Chini ya katiba mpya,rais huapishwa rasmi tarehe 20 mwezi Januari ya mwaka unaofuata baada ya uchaguzi.
Baadhi ya majimbo mengine ambayo hujulikana kama ''swing states'' ni pamoja na: Ohio,Virginia,Colorado,Carolina Kaskazini na Nevada.
0

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

HIVI NDIVYO BIASHARA YA NGONO NAMNA INAVYOTIKISA MOROGORO: SEHEMU YA PILI.

WAPENZI WANASANA WAKIFANYA MAPENZI GESTI

ANGALIA PICHA NDEGE KUBWA YA ABIRIA DUNIANI ILIYOANZA SAFARI NDEFU ZAIDI!

LICHA YA UZURI WAKE MWANADADA ELIZABETH MICHAEL a.k.a LULU SI MALI KITU MBELE YA RAY, AMKWEPA KUOGOPA AIBU.

ZIARA YA KATIBU MKUU WA CCM NDUGU KINANA NDANI YA CHAKE CHAKE,MKOA WA KUSINI PEMBA LEO.

IJUE HISTORIA YA UHASIMU WA KOREA KASKAZINI NA MAREKANI

MATOKEO YA DARASA LA SABA YATANGAZWA

NCHI YA URUSI NDIYO NCHI INAYOONGOZA KWA KUWA NA UBORA WA ELIMU NA VYUO DUNIANI.

TFF YATANGAZA MAJINA YA WACHEZAJI 30 WATAKAOWANIA TUZO YA MCHEZAJI BORA MSIMU HUU