Ujenzi wa reli mpya Tanzania kuharakishwa



Rais wa Tanzania Dkt. John Magufuli akiagana na Naibu Waziri wa Biashara kutoka China Qian Keming baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu, Dar es Salaam.Image copyrightIKULU, TANZANIA
Image captionRais wa Tanzania Dkt. John Magufuli akiagana na Naibu Waziri wa Biashara kutoka China Qian Keming baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu, Dar es Salaam.
Mradi wa ujenzi wa reli ya kati nchini Tanzania unatarajiwa kuharakishwa kufuatia mazungumzo kati ya Rais John Magufuli na Naibu Waziri wa Biashara wa China Qian Keming.
Reli hiyo ya kati ni ya kutoka Dar es Salaam, Mwanza, Kigoma na inatarajiwa kuunganisha Tanzania na nchi za Rwanda na Burundi
Wakati wa mazungumzo ikulu Dar es Salaam Rais Magufuli alisema serikali inataka kuona mambo yakifanyika na kutoa matokeo bila kupoteza muda, kwa mujibu wa taarifa kutoka ikulu.
Serikali ya Tanzania imetenga shilingi trilioni moja kwa ajili ya kuanza kwa ujenzi katika bajeti ya sasa.
"Sisi tumeamua kuanza ujenzi na tayari Wakandarasi 32 wamejitokeza kuomba kujenga reli ya kati kuanzia Dar es Salaam hadi Morogoro umbali wa kilomita 200 za mwanzo na tutatumia fedha zetu wenyewe," alisema Dkt Magufuli kwa mujibu wa taarifa kutoka ikul..
"Kazi hii tunataka ianze mwaka huu wa fedha, kwa sababu upembuzi yakinifu na usanifu umeshafanyika, kwa hiyo na nyie ongezeni kasi ili mradi huu wote ukamilike, nataka uwe umekamilika kabla sijaondoka madarakani."
Dkt Magufuli alisema mradi huo una manufaa makubwa kwa Tanzania na nchi nyingine nane zinazotegemea bandari ya Dar es Salaam na kwamba kukamilika kwake kutatoa mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi wa Tanzania ambayo inataka kuwa nchi ya kipato cha kati ifikapo mwaka 2025.
Kwa mujibu wa taarifa ya ikulu, Bw Qian aliahidi kuwa Serikali ya China itaongeza msukumo katika uharakishaji wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa reli hiyo ya kati.
"Mheshimiwa Rais Magufuli nimeielewa dhamira yako na kiu uliyonayo, naona kabisa kwamba dhamira ya kisiasa ipo ya kutosha, tunachotakiwa kukifanya ni kuwasukuma wataalamu wetu waongeze kasi," alisema.
„Na mimi nakuahidi kuwa tulikuwa tunakwenda kwa kasi ya kilometa 100 kwa saa, sasa tutaongeza na kwenda kilometa 200 kwa saa."

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*